Ngumi za kisultani kupigwa safari ya beach
DAR ES SALAAM: Bondia Sultani Kiyoko ametamba kumtwangaΒ Fransic Nampumula wa Mbagala kwenye pambano la safari ya Beach linarotarajiwa kupigwa Oktoba 22, 2023, Rongoni Beach Kigamboni Jijini Dar es salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati akiendelea na maandalizi Bondia Sultan Kiyoko amesema mazoezi anayofanya ni zaidi ya kucheza raundi sita.
“Nitakachofanya ni zaidi ya kucheza raundi sita walizo saini hivyo mpinzani afanye mazoezi ya kutosha ya kupokea kipigo cha aina yake siku hiyo.”amesemaΒ Bondia Kiyoko
Saidi Omar ni mdau wa masumbwi ambaye ni shabiki wa Kiyoko amesema “damu zitamwagika ulingoni kwa mpinzani waoΒ baada ya kupokea kichapo kitakacho pelekea kutotamani kucheza ngumi maisha yake yote.”amesema.



