Aslay Mihogo aeleza changamoto za wafanyabiashara

DAR ES SALAAM: Mjasiriamali na mdau wa biashara, Aslay Mihogo, amesema kuwa pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara nchini, bado wajasiriamali wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohitaji kupewa kipaumbele ili kuwawezesha kukuza biashara zao na kuongeza mchango wao katika uchumi.

Akizungumza kuhusu hali ya ujasiriamali nchini, Aslay amesema changamoto kubwa inayowakabili wafanyabiashara wengi ni upatikanaji wa mitaji yenye masharti nafuu, gharamaza uendeshaji wa biashara pamoja na changamoto ya kupata masoko ya uhakika kwa ajili ya bidhaa na huduma wanazozalisha.

Amesema kuwa mitaji ni nguzo muhimu kwa biashara yoyotekukua, lakini wajasiriamali wengi hasa wanaoanza safari yabiashara hukutana na vikwazo katika kupata fedha zakuendeleza shughuli zao kutokana na masharti ya mikopo kutokuwa rafiki kwa baadhi yao.

“Changamoto kubwa ni upatikanaji wa mitaji yenye mashartinafuu, gharama za uendeshaji wa biashara, na upatikanaji wamasoko ya uhakika. Ningependa Serikali iendelee kufanya tafitina kuboresha maeneo haya ili biashara ziweze kukua kwa kasizaidi na kuongeza ajira,” amesema Aslay.

Ameeleza kuwa Serikali ikiendelea kuboresha mifumo ya utoajiwa mikopo nafuu na kuweka mazingira bora kwawafanyabiashara, hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi yabiashara zinazofanikiwa na kutoa nafasi zaidi za ajira kwa vijanana makundi mengine katika jamii.

Kwa mujibu wa Aslay, biashara nyingi zina uwezo mkubwa wakukua lakini zinahitaji msaada wa kimkakati katika maeneomuhimu kama upatikanaji wa fedha, elimu ya biashara, teknolojia na fursa za masoko ili ziweze kushindana katika mazingira ya sasa.

Amesema kuwa amefaidika kutokana na maboresho yanayoendelea kufanyika katika mazingira ya biashara, hususan kupitia mafunzo, upatikanaji wa taarifa na fursa mbalimbali za uwezeshaji zinazotolewa kwa wajasiriamali.

“Nimefaidika kwa kuona mazingira ya biashara yameendelea kuboreshwa kupitia mafunzo, upatikanaji wa taarifa na fursa mbalimbali za uwezeshaji,” amesema.

Hata hivyo, Aslay amesisitiza kuwa bado kuna haja yakuendelea kurahisisha upatikanaji wa mitaji nafuu ili kuwapa nafasi wajasiriamali wengi zaidi kuanzisha na kupanua biashara zao bila kukabiliwa na changamoto kubwa za kifedha.

Ameongeza kuwa kupunguza urasimu katika baadhi ya hudumaza biashara ni hatua nyingine muhimu itakayosaidia wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi nakutumia muda mwingi katika kukuza biashara zao.

Kwa upande wa mafunzo, Aslay amesema kuwa kuna umuhimuwa kuongeza mafunzo ya vitendo kwa wajasiriamali ilikuwasaidia kupata ujuzi wa kusimamia biashara, kutengeneza mikakati ya masoko na kutumia teknolojia katika kuongeza tija.

Amesema kuwa ujasiriamali una nafasi kubwa katika kutatua changamoto ya ajira nchini, hivyo jitihada za kuwawezesha wajasiriamali zinapaswa kuendelea kupewa kipaumbele nakushirikisha wadau mbalimbali.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mifumo itakayowaunganisha wajasiriamali na masoko makubwa ilibidhaa zinazozalishwa ziweze kuwafikia walaji wengi zaidi nakuongeza kipato cha wafanyabiashara.

Amesema kuwa mazingira bora ya biashara yatawapa nafasi vijana wengi kuona ujasiriamali kama njia ya kujiajiri, kuajiriwengine na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wataifa.

Aslay ametoa wito kwa Serikali kuendelea kusikiliza maoni yawajasiriamali na kufanya maboresho yanayolenga kuondoa vikwazo vinavyokwamisha ukuaji wa biashara ndogo na za kati.

Ameeleza kuwa kwa kuwepo kwa ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za fedha na sekta binafsi, Tanzania inaweza kuwa namazingira imara zaidi ya biashara yatakayochochea ubunifu, uwekezaji na ajira kwa wananchi wengi zaidi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button