TBS yatoa mafunzo ya viwango Maonesho ya Madini Lindi

LINDI; Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kuwa karibu na wajasiriamali wadogo nchini kwa kutoa elimu kuhusu viwango na ubora wa bidhaa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha kuzalisha bidhaa salama, zenye ubora na zinazoweza kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
TBS imetoa elimu hiyo katika Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Lindi 2026, yanayofanyika Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi, ambapo wadau mbalimbali wamepata fursa ya kujifunza kuhusu viwango, taratibu za ubora wa bidhaa pamoja na umuhimu wa kuzingatia matakwa ya viwango katika uzalishaji na biashara.
Akizungumza katika maonesho hayo, Mhandisi Hemedy Hamim, Mkaguzi wa TBS Kanda ya Kusini, amesema TBS imeendelea kuwafikia wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia elimu inayolenga kuwawezesha kuboresha bidhaa zao na kuingia katika masoko yenye ushindani.
Katika utekelezaji wa jukumu hilo, TBS imewatembelea na kuwapatia elimu wajasiriamali wanaojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa za korosho, mafuta ya mwani, sabuni za mwani pamoja na Shower Jelly zinazotokana na mwani, huku ikiwahamasisha kuzingatia viwango vya ubora katika uzalishaji wao.
Hemedy amesema elimu hiyo pia inalenga kuwawezesha wajasiriamali kuelewa taratibu za kupata Alama ya Ubora ya TBS, ambayo ni muhimu katika kujenga uaminifu wa bidhaa kwa watumiaji na kuongeza uwezo wa bidhaa kufikia masoko mbalimbali.

TBS imeeleza kuwa kwa wajasiriamali wadogo, upatikanaji wa Alama ya Ubora unatolewa bila malipo, jambo linalolenga kuwawezesha wafanyabiashara hao wadogo kupata huduma za viwango na kuimarisha ubora wa bidhaa zao.
Katika kuwafikia kwa urahisi zaidi wajasiriamali hao, TBS imeshirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), ambapo ushirikiano huo umewezesha elimu ya viwango kuwafikia wajasiriamali wadogo wanaozalisha bidhaa mbalimbali, ikiwemo zile zinazotokana na mazao yanayopatikana katika maeneo yao.
TBS imewasisitiza wajasiriamali kutumia fursa hiyo kwa kuhakikisha bidhaa zao zinafuata taratibu zinazotakiwa na kupata Alama ya Ubora, kwani hatua hiyo inaweza kuongeza uaminifu wa bidhaa kwa walaji na kuwawezesha kutafuta fursa za masoko mapana zaidi.

Mmoja wa wajasiriamali walionufaika na elimu na huduma za TBS, Zena Adam, mbanguaji wa korosho kutoka Nachingwea, ambaye baada ya kufuata taratibu zilizowekwa na TBS alifanikiwa kupata Alama ya Ubora kwa bidhaa yake.
Zena ameishukuru TBS kwa elimu na maelekezo aliyopatiwa katika hatua mbalimbali, akieleza kuwa mafunzo hayo yamemsaidia kuelewa umuhimu wa ubora na taratibu zinazotakiwa katika uzalishaji.
Kwa mujibu wa Zena, kupata Alama ya Ubora ya TBS ni hatua muhimu kwake kama mjasiriamali, kwani anaamini itasaidia kuongeza uaminifu wa bidhaa zake na kumfungulia fursa za masoko kutoka nje ya Mkoa wa Lindi hadi katika masoko ya kimataifa.
Kwa upande wake, Fatma Machalila, ambaye ni miongoni mwa wajasiriamali walionufaika na elimu hiyo, ameipongeza TBS kwa kuendelea kuwafikia wajasiriamali wadogo na kutoa elimu kuhusu uzalishaji wa bidhaa bora.
Ushiriki wa TBS katika Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Lindi 2026 umeendelea kuonesha umuhimu wa taasisi hiyo kuwa karibu na wazalishaji na wajasiriamali, si kwa kutoa huduma za viwango pekee, bali pia kwa kutoa elimu inayowawezesha kuelewa namna ubora unavyoweza kuwa sehemu muhimu ya ukuaji wa biashara zao.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com
I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do….. https://www.work27.info