Balua atua Simba SC

KLABU ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Edwin Balua kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Tanzania Prisons.

Balua (23)anayetumia mguu wa kushoto anaweza kucheza winga zote.

Balua anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Simba dirisha dogo la usajili.

Mpaka sasa imesajili, Omar Jobe na Freddy Michael Kouablan.

Hata hivyo wameachana na wachezaji sita ambao ni, Jean Baleke, Moses Phiri, Jimmyson Mwanuke, Shaban Chilunda, Nassoro Kapama na Mohammed Mussa.

Habari Zifananazo

Back to top button