CCM Kilimanjaro yatoa neno mvua za El-Nino

KILIMANJARO; Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kukabiliana na mvua kubwa El Nino kwa kuhakikisha mitaro na mifereji inakuwa wazi na mikondo ya maji inaachwa ipite kwa usalama.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boi Safi, ambaye amesema maandalizi ya mapema ni muhimu katika kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
Amesema wananchi wanapaswa kushirikiana na uongozi wa Mkoa, wilaya na halmashauri katika kuzibua mifereji na mitaro, pamoja na kuondoa vikwazo katika maeneo ambayo maji hupita ili kuzuia mafuriko.
Patrick amesema wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni wanapaswa kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya mamlaka, ikiwemo kuhama katika maeneo hatarishi endapo wataelekezwa kufanya hivyo.
“Watabiri wa hali ya hewa wameshatoa tahadhari, hivyo ni vizuri tukajiandaa kungali mapema. Kuzibua mifereji na mitaro ni jambo moja, lakini pia tunapaswa kuhakikisha maeneo ambayo maji yanapita yanaandaliwa vizuri ili maji yaweze kupita kwa usalama,” amesema.
Aidha, amewataka wananchi kujiandaa kwa upatikanaji wa chakula, akisisitiza umuhimu wa kutumia vizuri kipindi cha mavuno kinachoendelea mkoani humo.
Amesema kwa sasa wakulima wanavuna mahindi, maharage na mazao mengine, hivyo wanapaswa kutenga sehemu ya mazao hayo kwa ajili ya akiba ya chakula badala ya kuuza yote.
“Kwa sasa Mkoa wa Kilimanjaro ni kipindi ambacho tunavuna. Tuna mahindi, tunavuna maharage na baadhi ya mazao mengine. Wananchi wajitahidi siyo kukimbilia tu kuuza, bali waweke akiba ya kutosha kwa kipindi hiki ambacho mvua hizi zinakadiriwa zinaweza kuendelea, ikiwezekana mpaka Januari,” amesema.
Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa maandalizi ya kukabiliana na mvua si jukumu la Serikali pekee, bali yanahitaji ushirikiano wa kila mwananchi, ikiwemo kutoa nafasi katika maeneo ambayo ni mikondo ya asili ya maji ili maji yaweze kupita bila kuzuiwa.
Amesema uongozi wa Mkoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri umeendelea kuchukua hatua za maandalizi, huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.




❤️ Wasichana warembo na wenye hamu ya kimapenzi kutoka kote duniani wanakungoja; jiunge hapa …………………………………………………………….………> https://da.gd/girls66