Helios yazindua maabara ya Tehama, wanafunzi 873 Kalenga kunufaika

Shule ya Sekondari ya Kalenga imepatiwa mbalimbali vya kisasa zikiwemo kompyuta za mezani 26, kifaa cha kuonyesha picha (projector),

IRINGA: JUMLA ya wanafunzi 873 na walimu 43 wa shule ya Sekondari Kalenga iliyopo katika katika Halmashauri ya Iringa wanatarajiwa kunufaika baada ya kampuni ya Helios Towers kuzindua maabara ya kisasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shule hiyo.

Mradi huo wenye thamani ya Shilingi milioni 30 umezinduliwa katika shule hiyo leo, Septemba 15, 2026 ikiwa ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo wa kurudisha kwa jamii kupitia uwekezaji katika sekta ya elimu na maendeleo ya kidijitali nchini Tanzania.

Ofisa elimu sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa, Alice Nkwera alizindua mradi huo na kueleza kuwa utasaidia kuongeza uelewa wa teknolojia, kuimarisha ujuzi wa kidijitali, na kuwaandaa kwa mahitaji ya soko la ajira katika dunia ya sasa inayotegemea teknolojia.

Mradi huo umefadhiliwa na Helios Towers Tanzania na kutekelezwa na Camara Education Tanzania, kwa ushirikiano wa karibu na uongozi wa shule pamoja na mamlaka za elimu za wilaya ya Iringa Vijijini na kuzinduliwa na Ndugu Alice, Afisa Elimu wilaya ya Iringa Vijijini.

SOMA: Shirika la Camara lazindua kituo cha kidijitali shule ya umma Nyasa 

Kupitia mradi huo, Shule ya Sekondari ya Kalenga imepatiwa mbalimbali vya kisasa zikiwemo kompyuta za mezani 26, kifaa cha kuonyesha picha (projector), luninga ya kidijitali (Smart TV), internet, ubao mweupe (whiteboard), vifaa vya matengenezo ya TEHAMA (maintenance kit), pamoja na miundombinu ya mtandao wa ndani (LAN).

Helios Towers Helios Towers ni kampuni ya kimataifa inayojihusisha na ujenzi na uendeshaji wa miundombinu ya minara ya mawasiliano katika nchi mbalimbali barani Afrika, ikiwemo Tanzania, kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuimarisha maendeleo ya kidijitali katika jamii.

Kampuni hiyo imeshirikiana na Camara Education Tanzania ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali inayoboresha elimu kupitia matumizi ya teknolojia kwa kusambaza vifaa vya TEHAMA mashuleni, kutoa mafunzo kwa walimu, pamoja na kusaidia shule kujenga uwezo wa matumizi ya kidijitali katika ufundishaji na ujifunzaji.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I do not even know how I ended up here, but I thought
    this post was good. I do not know who you are but definitely you
    are going to a famous blogger if you are not already ;
    ) Cheers!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button