CCM yampendekeza Ndejembi kumrithi Nchimbi
DAR ES SALAAM – Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempendekeza Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia kujiuzulu kwa Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.
Pendekezo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za CCM, Lumumba, Dar es Salaam.
Nchimbi alijiuzulu nafasi hiyo kuanzia Septemba 4, 2026, na Rais Samia Suluhu Hassan amekubali ombi hilo. Serikali ilisema taratibu za kikatiba za kumpata Makamu wa Rais mwingine zitafuatwa.



