NAIBU Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko kwa kuungana na mfuko wa Abbott amezindua shule ya sekondari Miles and Kimberly iliyopo eneo la Mapatano Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga Oktoba 1, 2024.
Shule hiyo iliyojengwa na kuboreshwa upya ina uwezo wa kupokea wanafunzi 800 wa kidato cha tano na sita, kwa michepuo ya sayansi.
Akizungumza katika mfunguzi wa shule hiyo, Dk Biteko amesema: “Nataka niwapongeze sana wadau wote mlioshiriki kwa hali na mali, na hususani Abbott Fund kwa namna mlivyojitolea, tunawashukuru sana kwa mchango ambao mmetoa kwenye jamii hii na tunashukuru sana kwa misaada yenu ambayo mmekua mkiitoa kwenye Jamii, tangu mmekuja hapa Tanzani.”
“Niwaombe wananchi wote tutunze miundombinu hii tuliyonayo inayowezesha kupatia elimu watoto wetu,” Dk Biteko ameongeza.
Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Abbott, Robert Ford amesema kwa kuzingatia suala la afya elimu ni msingi wa maendeleo na ustawi ndio maana wamefanya elimu kuwa lengo kuu la ushirikiano wao wa muda mrefu nchini Tanzania.
SOMA: Dk Biteko azindua mpango wa ujuzi kidigitali
“Tukichukuliwa pamoja na kazi yetu ya kuimarisha fursa za afya na kiuchumi, tunatumai uwekezaji huu katika elimu utasaidia watu wengi zaidi nchini Tanzania kuishi maisha yao kikamilifu,” amesema