KCMC waja na mpango kukakabili magonjwa ya kuambukiza

KILIMANJARO; Katika juhudi za kuimarisha uwezo wa Tanzania kwenye utafiti wa afya na mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, Chuo Kikuu cha KCMC kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini Denmark kimezindua mpango maalumu wa kuwajengea uwezo wataalamu wake katika eneo la kinga ya mwili na utengenezaji wa chanjo.
Mpango huo unalenga kuzalisha wataalamu wasiopungua 16 katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka 2026 hadi 2032, watakaokuwa na ujuzi wa kufanya tafiti za kinga ya mwili na utengenezaji wa chanjo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika Agosti 13, 2026, Mtafiti Kiongozi na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu KCMC, Dk Godfrey Temba, amesema Tanzania bado ina idadi ndogo ya wataalamu katika eneo la kinga ya mwili na utengenezaji wa chanjo, licha ya kuwa na uhitaji mkubwa wa wataalamu wenye ujuzi katika sekta hiyo.
“Katika mpango ambao tumeuzindua leo, Chuo Kikuu cha KCMC, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Ghana pamoja na Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini Denmark, tutaandaa wataalamu kutoka Tanzania kila mwaka. Nchi zetu zina uhitaji mkubwa wa kujenga uwezo wa wataalamu wetu ili waweze kutambua, kubaini na kujifunza namna ya kutengeneza chanjo,” amesema Dk Temba.
Amesema kundi la kwanza la wataalamu watatu litaondoka nchini wiki ijayo kuelekea Denmark, ambako litakaa kwa miaka miwili likijifunza kuhusu kinga ya mwili na namna ya kutengeneza chanjo kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.
Kwa mujibu wa Dk Temba, programu hiyo itatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo kila mwaka wataalamu watatu hadi wanne kutoka Tanzania watapelekwa Denmark kwa ajili ya mafunzo hayo.
“Watakapokwenda na kupata mafunzo, watarejea nchini kwa ajili ya kushirikiana na wataalamu wengine na kuimarisha eneo hili la utafiti na utengenezaji wa chanjo,” amesema.
Aidha, amesema KCMC ina mpango wa kuanzisha programu ya Shahada ya Uzamili (Masters) itakayolenga kuwaandaa wataalamu katika maeneo ya kinga ya mwili na chanjo.
“Uhitaji wa wataalamu wa chanjo nchini ni mkubwa sana, hasa katika eneo la kinga ya mwili ambalo ndilo linalomwandaa mtaalamu kuelekea katika utengenezaji wa chanjo. Tuna wataalamu wachache sana katika eneo hili, hivyo tunahitaji kuongeza idadi yao,” amesema.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu KCMC, Profesa Kajiru Kilonzo, amesema mafunzo hayo yatasaidia kuongeza uwezo wa wataalamu katika ubunifu na kuibua mawazo mapya yatakayoweza kusaidia kutatua changamoto zinazolikabili taifa.
“Mafunzo haya yatasaidia kubadilisha jamii katika ubunifu na kuwa na mawazo tofauti. Wale ambao wamechaguliwa mahususi watafundishwa zaidi kuhusu jinsi ya kugundua vitu vipya,” amesema Profesa Kilonzo.
Kwa upande wake, mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini Denmark, Profesa Lea Barford, amesema ushirikiano kati ya taasisi hiyo na Tanzania utasaidia kuimarisha uwezo wa wataalamu katika eneo la kinga ya mwili na chanjo.

“Tumeshirikiana na KCMC kwa miaka mingi katika masuala mbalimbali ya utafiti, zaidi ya miaka 20, hivyo tunaamini ushirikiano huu utaleta mafanikio makubwa katika sekta hii,” amesema.
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wa programu hiyo, Dk Immaculate Gabriel amesema maendeleo ya teknolojia yanaweza kuiwezesha Tanzania kufikia hatua ya kutengeneza chanjo zitakazotumika si nchini pekee bali pia katika maeneo mengine duniani.
“Sasa hivi tumekuwa na magonjwa mengi ambayo hayana chanjo, magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza. Kupitia mafunzo haya tunatarajia kujenga na kuimarisha uwezo wa kutengeneza chanjo sisi wenyewe,” amesema.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ Payathome1.com
Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ https://Www.Payathome1.com