Kihenzile: watumishi wazembe ATCL wachukuliwe hatua

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuwachukulia hatua watumishi wanaoshindwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kihenzile ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wafanyakazi wa ATCL, ambapo amesisitiza umuhimu wa watumishi kuwaheshimu na kuwahudumia wananchi kwa weledi.

Amesema mtumishi yeyote anayemdharau mwananchi anakuwa anachangia kuleta mgogoro kati ya Serikali na wananchi wake.

“Huko mtaani kuna watu wenye sifa kuliko sisi na hawana kazi. Tumepata nafasi hii, hivyo tuitumie vizuri kwa kutoa huduma bora,” amesema Kihenzile.

Aidha, Naibu Waziri huyo amemeelekeza Shirika la Ndege la Tanzania kuandaa mpango wa ziada wa kuongeza idadi ya ndege ili kuongeza uwezo wa shirika hilo na kukuza shughuli zake.

Amesema mpango huo haupaswi kutegemea pekee Serikali kununua ndege, bali uzingatie pia njia mbadala kama kukodi au kununua ndege kwa mipango ya kibiashara.

“Mje na mpango wa ziada, sio wa kutegemea Serikali inunue ndege pekee; iwe ni kukodi au kununua,” amesisitiza Kihenzile.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button