Kikwete asisitiza elimu kwa wazabuni makundi maalum

ARUSHA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amewaagiza maofisa manunuzi na wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali nchini kutoa elimu ya zabuni kwa makundi maalum, vijana na wanawake ili waweze kuomba zabuni na kujikwamua kiuchumi.

Ridhiwani ametoa agizo hilo jijini Arusha kwenye kufunga kongamano la 9 la ununuzi wa lililoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma(PPRA)  na kushirikisha washiriki zaidi ya 1500 kutoka mamlaka ya ununuzi wa umma

Amesema wananchi  bado hawajui maana ya asilimia 30 ya uombaji wa zabuni badala yake asilimia wanayoijua ni  kumi katika mikopo inayotolewa na halmashauri mbalimbali nchini.

“Shirikisheni madiwani, wabunge na wenyeviti wa halmashauri ili wajue uwepo wa asilimia 30 ya manunuzi na kuwaeleza wananchi ili waweze kuomba zabuni na kujikwamua katika uchumi wa kidigitali kwani mfumo wa NeST umewezesha sekta ya ununuzi kukua kwa kasi”

SOMA ZAIDI

PPRA yatakiwa kuendeleza mafanikio

Amesisitiza mafunzo ya kibiashara kwa vijana na watu wenye ulemavu ni muhimu ili wajikwamue kiuchumi kwani wanawake katika ukopaji wameonekana kuwa vinara wa kurejesha mikopo kwa wakati.

“Anzisheni programu shirikishi kati ya sekta binafsi na umma kwa ajili ya uanagenzi na ujuzi ili kuwezesha makundi maalum kupata zabuni ili kujikwamua kiuchumi na kusisitiza watu wenye ulemavu wapewe fursa za kupata zabuni wakiwemo vijana ili wajikwamue kiuchumi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button