Kyerwa yakamilisha jengo la mama na mtoto Rukuraijo

KYERWA: Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera imekamilisha ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Zahanati ya Rukuraijo kwa gharama ya Sh milioni 300, fedha zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Jengo hilo linatarajiwa kutoa huduma kwa wakazi wa Kata ya Rukuraijo ambao ni zaidi ya 9,000, huku likilenga kupunguza changamoto ya akina mama kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kujifungua.
Baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamesema kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kuondoa tatizo la akina mama kujifungulia njiani, hali ambayo ilikuwa ikihatarisha maisha ya mama na mtoto.
Wamesema awali baadhi ya wajawazito walilazimika kupelekwa katika Kituo cha Afya Nkwenda kwa ajili ya huduma za kujifungua, safari ambayo ilichukua muda mrefu na kuongeza hatari kwa mama na mtoto.

Akitoa taarifa mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwango’nda, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Rukuraijo, Datius Rukola, alisema mradi huo unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya ya uzazi na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika vituo vya afya vya kata na wilaya.
Alisema jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2024 na limekamilika kwa lengo la kuhakikisha wakazi wa Rukuraijo wanapata huduma za uzazi kwa urahisi na kwa wakati.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwango’nda, ameipongeza Halmashauri ya Kyerwa kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.
Mwango’nda ameshauri Halmashauri hiyo kujenga pia jengo la upasuaji katika zahanati hiyo ili kuongeza wigo wa huduma na kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki za afya katika eneo lao.
Zahanati ya Rukuraijo ni miongoni mwa miradi sita iliyopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Kyerwa, yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 3.9.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com