Mashindano ya KNK yaibua vipaji Bukombe

GEITA; Jumla ya vijana 6,100 kutoka timu 248 wamepata fursa ya kuonesha vipaji vyao katika msimu wa 10 wa mashindano ya Kusema Na Kutenda (KNK) Cup 2026, wilayani Bukombe mkoani Geita.

Mashindano hayo yamefanyika katika kata 17, za wilaya ya Bukombe, ambapo jumla ya mechi 342 zilichezwa na kuhitimishwa na mchezo wa fainali kati ya Ushirombo Warrors na Katome FC.

Mchezo huo wa fainali ulichezwa Septemba 7, 2026 katika uwanja mpya wa halmashauri ya Bukombe na Ushirombo Warriors waliibuka mabingwa wa mashindano ushindi kwa mabao 2-0.

Katibu wa Mashindano ya KNK CUP 2026, Jenifer Kisusi amesema rmashindano mwa kwaka huu yalianza Julai 3, 2026.

“Kujengewa uwanja wa michezo wa kisasa imekuwa ni chachu kwa wanamichezo na jamii kujihusisha na masuala ya kimichezo sambamba na kuchochea fursa za kiuchumi,”amesema.

Mratibu wa mashindano hayo, Bosco Mwidadi amesema kuwa mpaka sasa mashindano hayo yamechezwa ndani ya miaka 10 mfululizo tangu yalipoasisiwa.

Amesema  tayari mashindano hayo yameshaonesha matokeo chanya kwa baadhi ya wachezaji kuitwa kwenye timu za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 17 na miaka 20.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka wilaya ya Bukombe, Ramadhan Mung’oi amesema mashindano yanajenga jukwaa la kupata wachezaji watakaosaidia kupata timu ya ligi kuu kutoka Bukombe.

“Malengo yetu ni kukusanya vijana ambao tutapenda kuwaendeleza katika mchezo wa soka ili kwa baadaye kuweza kupata timu ya ligi kuu kutoka wilaya ya Bukombe,” amesema Mung’oi.

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano KNK CUP 2026, Joseph Msimba amesema kupitia mashindano hayo wana matumaini ya kupata wachezaji wengi kutoka nje ya Bukombe.

Nahodha wa timu ya Katome FC, Paschal Paul amekiri kuwa mashindano hayo yametoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji vyao, huku akiomba eneo la waamuzi kuendelea kuboreshwa zaidi

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button