Mbio za nishati safi ya kupikia kuiteka Arusha

ARUSHA: MSIMU wa kwanza wa Mbio za ‘Clean Cooking half Marathon’ zinatarajiwa kufanyika Agosti 3, 2025 eneo la Njiro, jijini Arusha.

Mbio hizo zitahusisha umbali wa kilomita 21, kilomita 10 na kilomita 5 lengo kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya nishati safi, salama, na endelevu kwa ajili ya kupikia katika kaya na jamii za Kitanzania.

Pia mbio hizo zitaambatana na mafunzo mbalimbali juu ya umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia na madhara ya kutumia nishati isiyo safi.

Pia wadau wa teknolojia mbali mbali za Nishati Safi watapata fursa za kuonesha bidhaa zao ambapo kauli mbiu mbiu ni ‘Nishati Safi ya Kupikia, Linda Afya, Hifadhi Mazingira kwa Uchumi Endelevu’.

SOMA ZAIDI

Ajenda ya nishati safi inavyoibeba Tanzania

Toleo la kwanza la mbio za Clean Cooking Marathon zilifanyika jijini Dar es Salaam, ambapo sasa ni zamu ya Kanda ya Kaskazini. Aidha kwa mujibu wa waandaaji kutakuwa na zawadi za majiko ya nishati safi ya kupikia ambazo zitatolewa kwa washindi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button