Mbunge ahoji mkakati kuipa hadhi taaluma ya udereva

DODOMA; Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi amehoji bungeni mkakati wa serikali kuhakikisha taaluma na kazi ya udereva inakuwa na staha, hadhi na heshima sawa na kada nyingine.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ofisi yya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray amesema serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha taaluma na kazi ya udereva inakuwa na hadhi na heshima sawa na kada nyingine.

“Ili kuhakikisha taaluma na kazi ya udereva inakuwa na staha, hadhi na heshima sawa na Kada nyingine, Serikali, pamoja na mambo mengine, imeendelea kuboresha Muundo wa Maendeleo ya Utumishi wa Kada hiyo, kuboresha mafunzo ya kitaaluma na viwango vya elimu, kuimarisha motisha na maslahi ya kada ya udereva ili kukidhi na kumudu mazingira ya utendaji kazi,” amesema Naibu Waziri.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button