Mtatifikolo atoa mil 1/- kwa kikundi cha wanawake Isimani

IRINGA: MBUNGE wa Jimbo la Isimani, Emmanuela Mtatifikolo, ametoa Sh milioni moja kwa kikundi cha wanawake cha Mwangaza Food Point katika Kijiji cha Mboliboli, Tarafa ya Pawaga, jimboni kwake Isimani, ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono kuongeza mtaji na kukuza shughuli zao za kiuchumi.

Pamoja na mchango huo, Mtatifikolo aliahidi katika kijiji cha Mbugani kusaidia upatikanaji wa pampu itakayowezesha kusukuma maji kutoka kisimani, huku akitoa Sh 500,000 kama mchango wa ununuzi wa mfumo wa sola utakaotumika kuendesha pampu hiyo.

Misaada hiyo imetolewa wakati wa ziara yake katika vijiji hivyo, ambako pia alisikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuanza kuchukua hatua za kuzitatua.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi cha wanawake, Mtatifikolo aliwapongeza kwa kujikusanya na kuanzisha shughuli za kiuchumi, akisema hatua hiyo inaweza kuongeza kipato cha familia, kuwawezesha kujitegemea na kutengeneza fursa za ajira kwa vijana.

Alisema jitihada za wanawake kushirikiana katika shughuli za uzalishaji ni sehemu muhimu ya kujenga uchumi wa kaya na jamii, hivyo ni muhimu kuendelea kuunga mkono vikundi vinavyoanzisha shughuli zenye tija.

Kwa upande wao, wanakikundi walimshukuru mbunge huyo kwa msaada huo, wakisema fedha walizopewa zitawawezesha kuongeza mtaji na kuimarisha shughuli zao.

Akiwa katika kijiji cha Mbugani, alipokea changamoto ya ukosefu wa maji ya uhakika kwa ajili ya mifugo.

Alisema anaendelea kufuatilia changamoto nyingine zilizowasilishwa na wananchi na kwamba atawashirikisha viongozi mbalimbali wa Serikali, wakiwemo mawaziri wenye dhamana ya kilimo na umwagiliaji, ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo.

Katika ziara hiyo, Mtatifikolo alitembelea Kituo cha Afya Mboliboli kwa ajili ya kukagua huduma zinazotolewa na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi pamoja na wahudumu.

 

Miongoni mwa changamoto alizobaini ni ukosefu wa umeme katika kituo hicho, hali inayokwaza utoaji wa baadhi ya huduma za afya.

Baada ya kubaini changamoto hiyo, mbunge huyo aliwasiliana kwa njia ya simu na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Iringa, akiomba hatua zichukuliwe kwa haraka ili kituo hicho kipatiwe umeme.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button