OTFA yaishukuru serikali kwa sapoti

DAR ES SALAAM: Kituo cha soka cha One Tanzanite Football Academy (OTFA) imerejea nchini ikiwa na mafanikio makubwa baada ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya vijana yaliyofanyika nchini Sweden na Denmark, huku ikitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa kuwawezesha kushiriki na kuwapa ushirikiano katika safari hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili nchini, Kocha wa OTFA, Adam John Mwakibibi, alisema akademii hiyo ilishiriki mashindano ya Gothia Cup nchini Sweden na Dana Cup nchini Denmark ikiwa na timu mbili za vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 na kikosi cha miaka 18/19.

Ameeleza kuwa katika mashindano ya Gothia Cup, timu ya vijana wa chini ya miaka 17 ilifanya vizuri na kutwaa ubingwa, huku kikosi cha miaka 18/19 kikifanikiwa kufika hatua ya timu 32 bora. Baada ya hapo walielekea Denmark kushiriki Dana Cup ambapo timu ya U17 ilifika hatua ya 16 bora, wakati timu ya miaka 18/19 ilimaliza mashindano ikiwa mshindi wa tatu.

Mwakibibi alisema mafanikio hayo si ya wachezaji waliosafiri pekee, bali ni ya familia nzima ya One Tanzanite Football Academy, wazazi, walimu, viongozi, vijana waliobaki nyumbani pamoja na Watanzania wote walioendelea kuwaunga mkono.

Aidha, alitoa shukrani maalum kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden, akisema uliwapokea, uliwahudumia na kuwapa ushirikiano mkubwa tangu walipowasili hadi ulipowasindikiza uwanja wa ndege walipokuwa wakirejea nchini.

“Kwa namna walivyotusimamia na kutuhudumia, tumepata imani kuwa Serikali yetu ilikuwa pamoja nasi katika kila hatua ya safari hii, kuanzia tulipoondoka Tanzania hadi tuliporejea nyumbani,” alisema Mwakibibi.

Kocha huyo alihitimisha kwa kueleza kuwa mafanikio hayo yanaendelea kudhihirisha uwezo wa vipaji vya vijana wa Tanzania kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na kuipeperusha vyema bendera ya taifa.

Naye Ofisa michezo, Petro Gallos Chelula Kutoka Baraza la Michezo Tanzania (BMT)amewapongeza timu hiyo kwa kurudi na makombe hayo na amehidi Serikali itatengeneza mazingira rafiki Katika kukuza vipaji vyao.

Nao Kwa upande wao, Said Rashid mchezaji na Ismail Elija Kapteni one Tanzanite ameshuru viongozi wazazi Serikali kwenda na kurudi salama na udhutu ni kupambana ,kunitumia ndio Siri ya mafanikio yao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button