Polisi Arusha wapanda miti Shule ya Msingi Arusha

ARUSHA: Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewakumbuka viongozi wakuu wa serikali pamoja na watu maarufu nchini waliosoma katika Shule ya Msingi Arusha, maarufu kama Arusha School, kwa kupanda miti ya matunda na kivuli katika eneo la shule hiyo.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya kuwaenzi viongozi na watu mbalimbali waliopata elimu katika shule hiyo kongwe kwa mchango wao mkubwa walioutoa kwa Taifa.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti katika Arusha School, shule iliyoanzishwa mwaka 1934, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Marijani Mrope, ambaye ni Mkuu wa Polisi Jamii Jiji la Arusha, alisema viongozi waliokumbukwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Thabit Kombo, mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji, pamoja na watangazaji Salum Kikeke na Millard Ayo.
Mrope alisema yeye pamoja na Polisi Kata wenzake na dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Arusha walifika shuleni hapo kwa ajili ya kupanda miti hiyo ikiwa na malengo mawili ya kutunza mazingira na kuenzi viongozi, mashujaa na watu mbalimbali waliopita katika shule hiyo maarufu.

Alisema Arusha School imekuwa kama mti mkuu uliootesha matawi yaliyoleta kivuli na matunda mema kwa Taifa na dunia kwa ujumla, hivyo upandaji wa miche hiyo unaonesha kuthamini mchango wa waliowahi kusoma katika shule hiyo.
Kwa mujibu wa Mrope, viongozi hao walikuwa kama mbegu ndogo zilizopandwa katika shule hiyo, zikakuzwa kwa maarifa na maadili, na baadaye kuwa miti mikubwa yenye kutoa matunda kwa jamii.
Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha Polisi Jamii linaamini kuwa usalama wa raia na mali zao unaendana pia na utunzaji wa mazingira.
“Mti mmoja tunaoupanda leo ni alama ya amani, ulinzi na maendeleo endelevu kwa nchi,” alisema Mrope, huku akiwaasa wanafunzi kuwa wao ni mbegu ya kesho na wanapaswa kufuata nyayo za waliowatangulia ili Taifa lijivunie uwepo wao.
Aliwataka Polisi Kata kushirikiana na jamii katika kuhakikisha miti hiyo inalindwa na kutunzwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake, mwanafunzi wa Arusha School, Shaban Ally, aliwashukuru Jeshi la Polisi kwa kufika shuleni hapo na kupanda miti hiyo, akisema hatua hiyo ni njia mojawapo ya kuwaenzi viongozi, watu maarufu na wafanyabiashara waliowahi kusoma katika shule hiyo.
Alisema miti hiyo itatunzwa na kuitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha katika kuhifadhi mazingira na kuenzi historia ya watu waliotoa mchango kwa Taifa.




ok9 cung cấp đa dạng các sản phẩm trò chơi giải trí như: bóng đá, bắn cá, nổ hũ… Cùng nhiều khuyến mãi ưu đãi hấp dẫn tại https://ok99678.com/
Jacqueline Patrick (Jack Patrick) — mwanamitindo/video model Mtanzania. Global Publishers iliripoti kwamba alikamatwa Hong Kong kwa kesi ya dawa za kulevya
Ashura — alitajwa kwenye taarifa ya Global Publishers kuhusu Mtanzania aliyekamatwa China pamoja na mume wake Baraka katika kesi ya dawa za kulevya. Chanzo hicho kinamtaja Ashura na Baraka, lakini taarifa hiyo haithibitishi wazi kwamba walikuwa wasanii.
Dossa — Mtanzania mwenye umri wa miaka 39 aliyekamatwa Macau mwaka 2020, akiwa na kilo 15 za cocaine na kilo nyingine 2.5 za dawa ambazo hazikutambuliwa wakati huo.
Watanzania 13 — Hong Kong Customs ilitangaza rasmi kwamba wanaume 13 kutoka Tanzania walikamatwa katika operesheni ya Novemba 2006, wakiwa wanadaiwa kuficha heroin mwilini. Mamlaka ilisema baadhi walijitambulisha kama mafundi seremala, wafanyabiashara, wachezaji mpira, mabondia, wanafunzi au wasio na ajira
Watanzania 11 — taarifa ya mwaka 2014 iliripoti kwamba Watanzania 11 walikamatwa Hong Kong kati ya Aprili na Mei 2014 katika kesi tofauti za dawa za kulevya. Majina yao hayakuwekwa wazi kwenye chanzo nilichopata.
Sandra Khan (“Binti Kiziwi”) — video vixen/model
Alijulikana Tanzania baada ya kuwa video vixen mkuu kwenye wimbo “Binti Kiziwi” wa Z-Anto.
Alikamatwa Hong Kong mwaka 2013 katika uwanja wa ndege baada ya dawa za kulevya kugunduliwa zikiwa zimefichwa tumboni mwake.
Alikaa takribani miaka miwili rumande, kisha akapatikana na hatia ya usafirishaji wa dawa za kulevya na kuhukumiwa miaka mitano jela.
Alimaliza kipindi chake cha kisheria Desemba 2019 na kurejea Tanzania Januari 2020.
Baadhi ya vyombo vya habari Tanzania viliripoti kifungo chake kama miaka saba au minane, lakini chanzo kinachoeleza mchakato kwa undani kinasema miaka miwili ya rumande + miaka mitano ya kifungo
Brayton N. Lyimo — Mtanzania mwenye umri wa miaka 31. Alikamatwa Delhi mwaka 2018 na Narcotics Control Bureau (NCB), akiwa na takribani kilo 4.8 za heroin kwenye mizigo yake
Mtwanzi Carlos Adam — Mtanzania aliyekamatwa Mumbai mwaka 2021 akiwa na tuhuma za kusafirisha cocaine iliyokuwa imefichwa mwilini. Alikamatwa pamoja na Rashid Paul Sayula. Serikali ya India ilithibitisha kukamatwa kwao.
Rashid Paul Sayula — Mtanzania aliyekamatwa pamoja na Carlos Adam huko Mumbai, India, Aprili 2021, katika kesi ya cocaine iliyofichwa mwilini.
Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com