Polisi wanawake Njombe watakiwa kutoa elimu ukatili

NJOMBE: MAOFISA, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wanawake mkoani Njombe wametakiwa kwenda kwa wananchi katika maeneo yao na kutoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya watoto, pamoja na kuhamasisha jamii kutoa taarifa za vitendo hivyo mapema.

Hayo yamesemwa Septemba 8, 2026, na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-Net), Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Kheriyangu Khamisi, wakati akihitimisha ziara yake ya kazi mkoani Njombe.

DCP Kheriyangu ametoa wito huo wakati alipokutana na wanachama wa TPF-Net Mkoa wa Njombe, ambapo aliwataka kuendelea kutumia nafasi zao kuwafikia wananchi na kutoa elimu ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto.

Ziara hiyo ya kazi ilianza Septemba 3, 2026, mkoani Songwe, ambapo DCP Kheriyangu alitembelea wilaya mbalimbali za mkoa huo, kisha kuendelea na mkoani Mbeya na kuhitimishwa Septemba 8, 2026, mkoani Njombe.

Katika ziara hiyo, DCP Kheriyangu amekutana na askari wanawake pamoja na viongozi wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto, kwa lengo la kuhamasisha utoaji wa huduma bora kwa jamii na kuimarisha jitihada za Jeshi la Polisi katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia na dhidi ya watoto.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button