PSSSF, TBN kuimarisha elimu kwa umma

DAR ES SALAAM: Timu ya maofisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imefanya ziara katika makao makuu ya muda ya Tanzania Bloggers Network (TBN), Kijitonyama jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujenga ushirikiano katika utoaji wa elimu kwa umma kuhusu hifadhi ya jamii, pensheni na uwekezaji.

‎Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa TBN, Beda Msimbe, amesema mtandao huo uko tayari kushirikiana na PSSSF katika kutoa na kusambaza elimu sahihi kwa wananchi kupitia majukwaa ya kidijitali.

‎Hata hivyo, amesisitiza umuhimu wa wanachama wa TBN kupewa mafunzo ya kina kuhusu shughuli na uendeshaji wa PSSSF ili waweze kufikisha taarifa sahihi kwa umma.

‎Kwa upande wake, Mkuu wa msafara wa PSSSF, Abdul Njaidi, amesema ziara hiyo inalenga kujenga uhusiano wa karibu na wadau wa habari pamoja na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii, hoja na maombi yaliyowasilishwa na TBN yatafanyiwa kazi ili ushirikiano huo uwe na manufaa kwa wananchi.

‎Njaidi amesema PSSSF inaona umuhimu wa kutumia vyombo vya habari vya kidijitali kufikisha elimu kwa wananchi wengi zaidi, hususan kuhusu masuala ya pensheni na uwekezaji unaofanywa na mfuko huo.



‎Naye Mdhamini wa TBN, Issa Michuzi, amesema mtandao huo unajivunia historia na weledi wake katika tasnia ya habari, akieleza kuwa TBN inaendelea kuhakikisha Tanzania inasomeka vyema katika medani za kidijitali kwa kusambaza taarifa zinazochochea maendeleo ya taifa.

‎Katibu wa TBN, Rahel Pallangyo, amesema mtandao huo uko tayari kutoa waandishi wake na kutumia majukwaa yake mbalimbali kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii na shughuli zinazotekelezwa na PSSSF.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button