MAKAMU wa Rais wa Tanzania, DK Philip Mpango amesema sababu ya kifo cha Edward Lowassa ni ugonjwa wa kujikunja utumbo, tatizo la mapafu na shinikizo la damu.
Akitoa taarifa hiyo leo kupitia TBC, Dk Mpango amesema kiongozi huyo ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu tangu Januari 14, 2022 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Dk Mpango amesema baada ya muda, Lowassa alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu na kurejea tena JKCI.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu , jamaa na marafiki wa kiongozi huyo kufuatia kifo hicho.