Serikali kuendelea kujenga mazingira bora kwa walimu

MOROGORO; Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuweka mazingira bora na salama ya kazi kwa walimu wote nchini na kushirikiana bega kwa bega na Chama cha Walimu Tanzania (CWT)na vyama vyote ambavyo ni halali vya wafanyakazi, ili kuimarisha amani na utulivu mahala pa kazi ambayo ndio chimbuko la ustawi wa kiuchumi na kijamii wa taifa.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu , Ajira, Kazi na Mahusiano, Dk Evaline Munisi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa makatibu wa mikoa na wilaya wa CWT nchini yanayofanyika kwa siku mbili mkoani Morogoro.
Dk Munisi amesema elimu ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi, kisayansi na kijamii na katika kipindi hiki cha awamu ya sita, serikali imefanya uwekezaji mkubwa usio na kifani.
Amesema serikali pia imeendelea kuajiri walimu wapya maelfu kwa maelfu, ili kupunguza uhaba wa walimu na kupunguza mzigo wa kazi kwa walimu waliopo.
Dk Munisi amesema elimu ndio msingi wa maendeleo yote ya kiuchumi, kisayansi na kijamii na katika kipindi hiki serikali imefanya uwekezaji mkubwa usio na kifani katika sekta ya elimu.

Amesema kuwa vyama vya wafanyakazi havikuundwa kwa ajili ya kusigana na waajiri, bali ni jukwaa la kisheria la kukaa meza moja na waajiri ili kujadiliana kwa hoja ,ushahidi , kuheshimiana na kupata suluhu ya pamoja.
Dk Munisi amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa na wa kipekee unaotolewa na walimu katika ujenzi wa taifa letu.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa CWT , Magesa Magesa amesema mafunzo hayo yanahusisha washiriki 240 na yamelenga kuwangezea uwezo kwemye masuala mbalimbali ya vyama vyya wafanyakazi na sheria zinazowahusu wafabnyakazi hususani kwa walimu.
Magesa amesema CWT imeendelea kuwa na ushirika na serikali katika kuboresha elimu , kujenga uwezo kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo na kuchangia uchumi wa taifa kupitia kodi na ajira pamoja na kuwakilisha taifa katika matukio mbalimbali ya kimataifa ya kielimu.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ https://Www.Payathome1.com