VETA, VTA kuendeleza ushirikiano mafunzo bora nchini

ZANZIBAR: MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeahidi kuendeleza ushirikiano na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar katika kutoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi yenye ubora kwa kwa wananchi wa pande zote mbili za Tanzania bara na Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema hayo Agosti 14 alipotembelea mabanda ya VETA na VTA katika Tamasha la Kizimkazi lililokuwa likifanyika katika viwanja vya Dimbani Kusini Unguja, Zanzibar.

“Niwashukuru wenzetu wa VTA kwa kuendelea kushirikiana nasi na tutahakikisha ushirikiano wetu unadumu na unazidi kuimarika siku hadi siku ili kuhakikisha wananchi wa visiwani na bara wanapata mafunzo ya ufundi stadi yenye ubora na yanayowawezesha kushiriki kikamilifu kwenye shuguli za kiuchumi na kijamii,” Alisema Kasore.

Kasore aliongeza kwa kusema, “tunamshukuru Rais kwa kutembelea banda letu kipindi cha tamasha hili, lakini pia tunashukuru kwa nguvu kubwa aliyoiweka katika upanauzi wa vyuo, tunawashukuru pia viongozi wengine wote waliopita na kututembelea na kutoa ushauri na maoni yao tumeyapokea na tutayafanyia kazi.”

Sambamba na hilo Kasore amesema VETA imepokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wahitimu wa VETA kuhusu kuongezwa kwa vyuo vinavyotoa mafunzo ya matengezo ya simu za mkononi pamoja na kuongeza muda wa kutoa mafunzo hayo kuwa mrefu na si muda mfupi pekee kama ilivyo sasa.

Kasore amehitimisha kwa kuishukuru Tasisi ya Mwanamke Initiative kwa kuipa VETA mwaliko wa kushiriki katika Tamasha hilo kwa kushirikina na VTA kwani imeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa visiwani ambao wamepata taarifa za kutosha kuhusu mafunzo ya ufundi stadi lakini pia huduma zitoleazo na vyuo vya VETA.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily…………
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ https://Www.Payathome9.Com

  3. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button