Sh milioni 769.5 zatumika mradi wa maji Mabira

KYERWA: Wananchi wa vijiji vya Mabira, Omukigando na Nyakatete, Kata ya Mabira wilayani Kyerwa, mkoani Kagera, wameondokana na adha ya kufuata maji umbali mrefu baada ya kukamilika kwa Mradi wa Maji Mabira.

Mradi huo umezinduliwa kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, hatua inayotarajiwa kumaliza changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji katika maeneo hayo.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kyerwa, Martin Philipo, amesema mradi huo umegharimu Sh milioni 769.5 na unalenga kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

Amesema hadi sasa katika Wilaya ya Kyerwa kuna vyanzo vya maji 37 vinavyotunzwa kwa uangalifu, ikiwemo chanzo kinachotumika katika Mradi wa Maji Mabira.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwango’nda, amewataka wananchi kushirikiana na viongozi wa Serikali katika kutunza miundombinu ya maji pamoja na kulinda vyanzo vya maji.

Aidha, amewataka wananchi kuhakikisha wanaunganisha huduma ya maji majumbani ili kupunguza muda wanaoutumia kufuata maji na kutumia muda huo katika shughuli nyingine za maendeleo.

Mwango’nda amesema utunzaji wa vyanzo vya maji na miundombinu ya miradi hiyo ni muhimu katika kuhakikisha huduma ya maji inaendelea kupatikana kwa wananchi kwa muda mrefu.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button