Vijana waanza kuikubali sekta ya kilimo

SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na India imeanza kuchukua hatua za kuendeleza sekta ya kilimo kwa kuandaa majukwaa yanayowaunganisha wadau, kubadilishana maarifa na teknolojia pamoja na kuibua fursa za ubia wa kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAB Group, Tahir Bari, amesema hayo leo, Septemba 3, 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa Maonesho ya 10 ya Kimataifa ya Kilimo Barani Afrika, yaliyoambatana na Maonesho ya Tatu ya Kilimo, Mifugo na Ufugaji wa Kuku.
Amesema amevutiwa na ushiriki mkubwa wa vijana katika maonesho hayo, akisema wengi wameanza kuiona kilimo kama biashara na wako tayari kujifunza na kutumia fursa zilizopo. Kufuatia matumizi ya teknolojia na mifumo ya kidijitali inaweza kuwawezesha vijana kuongeza tija hata katika mashamba madogo bila kuhitaji mtaji mkubwa.
Hatahivyo amesema upatikanaji wa teknolojia hizo pamoja na majukwaa ya kuwaunganisha wadau unaweza kuongeza ushiriki wa vijana katika kilimo na kukifanya kuwa sekta yenye ushindani na fursa kubwa za biashara. SOMA: Wawekezaji wavutiwa sekta ya kilimo



