Waathirika mvua Mikindani watakiwa kuwa wavumilivu

MKUU wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amewataka wananchi waliyopatwa na athari mbalimbali kwenye Manispaa ya Mtwara Mikindani ikiwemo kuingaliwa maji kwenye makazi yao kufuatia mvua zinazonyesha kuendeelea kuwa wavumilifu katika kipindi hicho.

Hayo yamejiri wakati Mkuu huyo wa Mkoa wa Mtwara kutembelea maeneo mbalimbali yaliyopata athari iliyotokana na mvua zinazonyesha mkoani humo.

Advertisement

Aidha lengo la ziara hiyo ni kuwapa pole wahanga wa tukio hilo na kuwataka waendelee kuwa wavumilivu katika kipindi hicho kwani serikali iko pamoja na wananchi hao.

Aidha, maji hayo yamepelekea uharibifu wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula, watu kukosa makazi hali iliyosababishwa na kuwepo kwa miundombinu isiyokuwa rafiki ya kuweza kuyatoa maji kutoka eneo moja kwenda sehemu nyingine.

Pia amewataka wananchi hao kuwa makini kwa kufata kununi za afya ili wasije wakapata magonjwa ya mlipuko na kupelekea kupata athari nyingine zaidi.

‘’Tumekuja kuangalia tuone hali halisi na kuwapeni pole, tutaangalia suluhisho la tatizo hili ambalo ni la muda mrefu ili liweze kukoma kabisa’’amesema Sawala.

Baadhi ya wananchi hao akiwemo Hadija Kalinge mkazi wa mtaa wa majengo kata ya chuno amesema changamoto inayopelekea athari hiyo kila mwaka kwenye maeneo yao ni kukosekana kwa mitaro ya kupitishia maji.

Mkazi wa mtaa wa kiyangu kata ya shangani, Zena Hassan ameiomba serikali kuwawekea miundombinu rafiki ili waweze kuondokana na adha hiyo ambayo ni ya muda mrefa sasa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *