Wahandisi wanawake watabasamu uongozi Samia
WAHANDISI wanawake nchini wamesema licha ya changamoto kadhaa walizonazo, ila uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umefanya kupunguza changamoto hizo na kuaminiwa pia.
Kauli hiyo wametoa ikiwa leo ni siku ya kongamano la tisa la wahandisi wanawake nchini Wanawake hao wamesema hivi sasa wamekuwa wakipewa nafasi za uongozi wa kusimamia miradi mikubwa ikiwemo ule wa ujenzi wa daraja la Magufuli.
Akizungumza na HabariLEO jijini Dar es Salaam Mhandisi Msimamizi wa Ujenzi wa Daraja la Magufuli lililoko Mkoa wa Mwanza kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROAD),Devota Kafuku amesema ni fahari kuwa msimamizi wa daraja hilo kwani miaka ya zamani wanawake walikuwa hawaaminiki katika nafasi hizo.
“Kwasababu hizi fani za uhandisi au wajenzi miaka ya nyuma waliamini wanaume kwahiyo kupewa nafasi na kuaminiwa kusimamia ni jambo la kujivunia tunafanya na hatuangushi.
Amesema hali hiyo inasaidia kuhamasisha wanawake wengi na kujua inawezekana kusimamia miradi mikubwa.
Amesema changamoto ni nyingi zimepungua kwani miaka ya nyuma hata kusoma na kutendea kazi unachokijua ilikuwa ni kazi hivyo sasa wanasoma na kuingia kazini.
“Kupewa nafasi inatutoa kwenye changamoto hamna mhandisi mwanamke ambaye amewahi kufanya vibaya wote wanafanya bidii na kuonesha mafanikio kama wanaume au na zaidi.
View this post on Instagram
Ameongeza “Uongozi wa Rais mwanamke umeongeza kujiamini zaidi kwa wahandisi wa kike na kutengeeneza mazingira hata wengine kuona wahandisi wanawake wanaweza imeamsha ari kuwa wanawake wanapopewa nafasi wanafanya kwa ujasiri.
Kwa upande wake Mhandisi Sisilia karangi ameeleza miongoni mwa changamoto ni kwenye familia kuna baadhi mhandisi mwananmke akiolewa muda wa kukaa na watoto na kuhudumia unakuwa mchache kutokana na kazi.
“Mfano sisi wa barabara muda mwingi unakuwa nje ya familia inahitaji moyo wa ziada na wa kuweka uwiano sawa ingawa sasa changamoto sio nyingi kama zamani sasa tunaenda site na wanaume na tunaenda mashuleni kuhamasisha watoto wa kike wasome masomo hayo.
Mhandisi Perpetua Kisamba Kutoka kurugenzi ya mipango idara ya ufuatiliaji TANROAD amesema wameweza kuleta wahandisi zaidi ya 170 kutoka mikoa 26 ya wakala ya barabara.
“Tunasimamia zaidi ya kilomita 37,000 za barabara kuu na za mikoa na wanawake wako katika nafasi mbalimbali ambao wanafanya kazi ya kusimamia na kujenga na kuhakikisha matengenezo ya barabara yanafanyika kwa ubora,”amefafanua.