Wapewa mafunzo matumizi mizani kidigitali

MAKARANI, maofisa ushirika na wenyeviti wa vyama vya msingi mbalimbali (AMCOS) mkoani Mtwara wamenolewa kuhusu matumizi ya mizani za kidigitali katika kuelekea msimu wa zao la korosho mwaka 2024/2025.

Mafunzo hayo yametolewa na kampuni inayojishughulisha na masuala ya usambazaji wa mizani hizo za kidigitali nchini ya Rotai yaliyofanyika katika manispaa ya mtwara mikindani mkoani humo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Ofisa Mauzo wa Kampuni hiyo ya Rotai Mussa Simba amesema Lengo la mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kuwapatia uelewa washiriki hao juu ya matumizi ya mfumo huo kwa ajili ya maandalizi ya upimaji wa korosho katika msimu huo.

‘’Zoezi hili litakuwa endelevu kidogo mapaka msimu ya korosho utakapoisha tutakuwa tunawapitia mara kwa mara kwa ajili ya kuendelea kuwarivyuu kidogo ili wazidi kuweza kumudu kutumia huu mfumo mbao ni wa kisasa na ni mfumo ambao ni mzuri’’

Ameongeza kuwa, ‘’Kwsasabau mzani huu hauwezi kumuibia mkulima wala kumpunja, pindi mkulima anapopeleka mzigo wake kwenye Amcos anapimiwa mzigo na anaona kilo zake kwenye mzani na anaona pale zenye uzito sahihi na pia anapata meseji kupitia simu yake kutokakana kilo zake,’’amesema Simba.

Hata hivyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo wazingatie mafunzo na waende wakafanyie kazi yao hiyo kwa weledi na uhakika zaidi kwa ajili ya upimaji wa zao hilo kwa wakulima.

Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Mtwara mikindani mkoani humo, Hamidu Omari ameishukuru serikali kwa mabadiliko hayo ya uendeshaji wa vyama hivyo vya ushirika hasa upande wa upimaji wa mazao kwasababu miaka mingi walikuwa wakipima mazao ya wakulima kwa kutumia mizani za kizamani (analogi).

Amesema mizani hizo zilikuwa hazileti uhalisia au uhalali wa yale mazao ambayo wakulima walikuwa wanapima kutokana zilikuwa hazitoi kilo halisi na kwamba mkulima alikuwa hapati kile ambacho anastahili kukipata lakini sasa kupitia mizani hizo za kisasa za kidigitali wakulima watapata uzito uliyokuwa sahihi katika mazao yao.

Mwakilishi kutoka Chama cha Msingi cha Dihimba Amcos iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani humo, Salima Mohamed ‘’Kwa nilivoelewa mimi kupitia mafunzo haya ni kwamba upimaji wa mazao kupitia mizani za zamani mkulima alikuwa anakosa haki yake kidogo ya msingi lakini hizi zilizoletwa sasa za kidigitali mkulima atafaidika na zao lake kwasababu atapima vizuri’’

Habari Zifananazo

Back to top button