Wasanii 19 kutumbuiza FuTopia Zanzibar

ZANZIBAR: WASANII na vikundi 19 kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Burundi, Mexico, Chile na Canada wanatarajiwa kupanda jukwaani katika msimu wa pili wa Tamasha la FuTopia.

Tamasha hilo litakalofanyika kwa siku mbili, Agosti 8 na 9 katika eneo la Fumba Town, Zanzibar limeandaliwa na Busara Promotions, waandaaji wa Sauti za Busara.

Mkurugenzi wa tamasha hilo, Journey Ramadhani alisema msimu wa mwaka huu unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi kuliko wa mwaka jana.

Alisema msimu huu utajumuisha wasanii wengi zaidi, programu zilizopanuliwa na fursa nyingi kwa wageni kufurahia ubunifu wa Afrika kupitia muziki, sanaa, chakula, afya, utamaduni, mazingira na michezo kwa rika zote kuanzia watoto hadi wazee.

Ramadhani alitaja orodha ya wasanii hao kuwa ni DJ Lag (Afrika Kusini), Vania Ice (Burundi), La Negra MeXa (Mexico), Sidi Blue Moon (Canada), Playroots (Chile), DJ Joozey na DJ Zoro.

Wengine ni Midimu Collective, Baba Kash & The Band, Brainboy & Tarazouk Band, GlobalLocal, Princekim, DCMA Taarab & Kidumbaki Ensemble, Rody Joh, Ngoma World, Sauti Marley, Zainooba, Hammer Q na Ruth Mlawa kutoka Tanzania.

Pamoja na orodha hiyo ya wasanii, Ramadhani alisema kuwa mbali na burudani za jioni, tamasha hilo litakuwa na shughuli mbalimbali za kijamii, maonesho, warsha za ubunifu na michezo kwa rika zote.

Alisema moja ya vivutio vya tamasha hilo ni shughuli zote za mchana zitakuwa za bure huku tiketi zikihitajika kwa matamasha ya jioni pekee.

“Tiketi za awali tayari zimeanza kuuzwa na waandaaji wanawahimiza wananchi na wageni kuzinunua mapema kabla ya bei za kawaida kuanza kutumika,” alisema.

Aliongeza: “Kutakuwa na warsha za ubunifu, maonesho ya sanaa, programu za utunzaji wa mazingira pamoja na shughuli nyingine za kijamii”.

FuTopia inafanyika katika mazingira ya Fumba Town, Zanzibar, ikiwa na lengo la kuunganisha muziki, ubunifu, biashara za ndani na utalii kupitia tamasha linalowakutanisha wasanii, wabunifu, wajasiriamali na jamii kutoka maeneo mbalimbali.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily…………
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button