Zuchu, Diamond waja kivingine kuelekea 40 ya mtoto

DAR ES SALAAM: Shamrashamra za kuelekea kuadhimisha siku 40 tangu kuzaliwa kwa mtoto wa mastaa wa muziki nchini, Zuhura Othman ‘Zuchu’ na Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, zimeendelea baada ya kufanyika kwa hafla maalum iitwayo Henna Day.
Hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwa mzazi wa Diamond, ilikuwa ya kuvutia na Zuchu alikuwa miongoni mwa wahusika wakuu wa tukio hilo.

Licha ya kupendeza kwa mavazi, Zuchu alionekana akiwakaribisha wageni, akiimba na kufurahia muziki pamoja na washiriki wengine wa hafla hiyo.
Wageni mbalimbali, wakiwemo mastaa, kama Nandy, Billnass, Jux, Rayvann na wengine wengi walijitokeza kushiriki hafla hiyo, huku baadhi yao wakichorwa henna, mapambo yanayopendwa na wanawake na yenye nafasi muhimu katika baadhi ya desturi na tamaduni.

Hafla hiyo ni sehemu ya shamrashamra zinazoendelea kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku 40 tangu kuzaliwa kwa mtoto wa Zuchu na Diamond Platnumz.




Thanks for this one. I’ve saved it for later because I know I’ll want to refer back to it — the kind of post that actually answers the questions people ask.
https://x.com/1988richmy
Great to see this covered properly. It’s a good starting point if you’re new to the topic. Looking forward to the next one.