Watu 34,139 wafikiwa mradi wa Buhoma

DAR ES SALAAM; WATU 34,139 kutoka vijiji 10 vya kata nne za Tarafa ya Makere, Halmashauri ya Wilaya Kasulu mkoani Kigoma, wamenufaika kupitia miradi mbalimbali ya kijamii iliyotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania iliyolenga kuboresha hali ya maisha na kipato cha wananchi wa maeneo hayo.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa mradi huo unaojulikana kama Mradi wa BUHOMA, Esther Mshendwa, wakati wa kufunga utekelezaji wa miradi hiyo kupitia ufadhili wa World Vision Marekani, ambayo imemamaliza muda wake na kusema utekelezaji wa miradi hiyo imeleta mabadiliko chanya katika vijiji vilivyonufaika na mradi huo kwa miaka 16 ya utekelezaji wake.

 Amesema World Vision imetoa madawati 1700 kwa shule za msingi, na vitabu 9783, kuwezesha  wanafunzi 7777 kujenga tabia ya kujisomea nyumbani na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba, huku vikundi 139 vya kuweka na kukopa vikiundwa.

 Amesema pia shirika hilo limejenga majengo ya chuo cha ufundi ambacho sasa kinatumika na VETA Kasulu, kujenga nyumba 197 kwa kaya masikini na kuwezesha wanafunzi 17,142 wa shule za msingi kupata huduma za vyoo bora.

 Akihitimisha miaka 16 ya utekelezaji wa mradi huo,  Mkuu wa Mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro ametaka mashirika yanayotekeleza miradi mbalimbali ya kijamii kuwa na matokeo yanayopimika na kuleta mabadiliko kwa jamii hasa kwenye kuinua kipato.

 Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya Kasulu, Kanali Isack Mwakisu, alisema kuwa  World Vision imekuwa mfano wa kuigwa kutokana na mafanikio mbalimbali na mabadiliko yaliyotokea kwenye jamii kutokana na miradi iliyotekelezwa ikiwemo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button