COPRA: Ingieni kilimo cha mkataba kwa wadau waliosajiliwa

dodoma; MAMLAKA ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), imewahimiza wakulima na wafanyabiashara wa mazao nchini kuhakikisha wanaingia katika kilimo cha mkataba kupitia wadau waliosajiliwa na mamlaka hiyo, ili kujiepusha na hasara na migogoro inayotokana na mikataba isiyo rasmi.
Rai hiyo imetolewa na Ofisa Kilimo na Mratibu wa Kilimo cha Mkataba kutoka COPRA, Rehema Msauge wakati wa kutoa elimu kwa wadau kuhusu kanuni za Kilimo cha Mkataba zilizotangazwa kwenye gazeti la Serikali Juni 30, mwaka huu.
Alisema kilimo cha mkataba kinachosimamiwa na COPRA kwa mazao yote yasiyo na bodi maalumu ni mfumo unaolenga kulinda maslahi ya wakulima na wanunuzi kwa kuhakikisha makubaliano yote yanatambulika kisheria na kusimamiwa ipasavyo.
Msauge alisema mikataba yote inapaswa kusajiliwa kupitia mifumo rasmi inayosimamiwa na COPRA na kutambuliwa na serikali za mitaa ili kuongeza uwazi, kuimarisha usimamizi na kurahisisha wakulima kupata mitaji, pembejeo pamoja na soko la uhakika.
“Hivyo wakulima na wafanyabiashara wanapaswa kuepuka makubaliano ya mdomo. Ni lazima wawe na mikataba ya maandishi inayotambulika kisheria, ambayo mamlaka itaisimamia ili kuondoa mazingira ya wakulima kudhulumiwa na kupata Hasara,” alisema.

Msauge alisema kabla ya kusainiwa kwa mkataba ni lazima kuwe na makubaliano ya awali yanayoonesha eneo la uzalishaji, taarifa husika zisajiliwe kwenye mfumo wa mamlaka, kisha rasimu ya mkataba iandaliwe, ihakikiwe na baadaye isajiliwe rasmi.
Alibainisha kuwa mfumo wa kilimo cha mkataba unampa mkulima uhakika wa soko kwa kuwa anafahamu mnunuzi wa mazao yake kabla ya mavuno, huku pia ukihakikisha upatikanaji wa bei yenye tija.
Msauge alisema COPRA huweka bei ya kuanzia ya mazao baada ya kufanya tathmini ya gharama halisi za uzalishaji na mwenendo wa soko, kwa lengo la kuhakikisha mkulima anapata kati ya asilimia 75 na 80 ya bei ya mwisho ya mazao husika.
Pia mfumo huo unaongeza fursa za wakulima kupata mikopo kutoka taasisi za fedha na wadau wa maendeleo kutokana na kuwepo kwa mikataba inayotambulika, pamoja na kuboresha ubora wa mazao kwa kuzingatia viwango vya soko la ndani na nje.

Kuhusu ada ya usajili wa mikataba, Msauge alisema mkulima mdogo atalipa ada ya Sh 10,000, mkulima wa kati Sh 20,000 na mkulima mkubwa Sh 40,000.
Alisema kwa vyama vya ushirika (AMCOS), vyenye wanachama kati ya 20 na 50 vitalipa Sh 100,000, vyenye wanachama 51 hadi 200 vitalipa Sh 250,000, huku vyenye wanachama 201 na kuendelea vikitozwa Sh 500,000.
Mamlaka hiyo pia imeonya kuwa ukiukwaji wa mikataba ya kilimo cha mkataba utachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni zilizopo.
Kwa mujibu wa kanuni hizo, mtu binafsi anayekiuka masharti ya mkataba anaweza kutozwa faini ya kati ya Sh milioni moja hadi Sh milioni tano au kifungo cha mwaka mmoja hadi miwili jela, au adhabu zote mbili kwa pamoja.
Kwa taasisi zinazokiuka masharti hayo, adhabu ni faini ya kati ya Sh milioni tano hadi Sh milioni 10.




This design is wicked! You most certainly know how
to keep a reader entertained. Between your wit and your videos, I was almost moved
to start my own blog (well, almost…HaHa!) Wonderful job.
I really enjoyed what you had to say, and more than that,
how you presented it. Too cool!