Kijaji aagiza TANAPA kujenga kituo udhibiti tembo

KAGERA: Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Ashatu Kijaji, ameiagiza Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Askari wa Uhifadhi wilayani Karagwe ili kudhibiti uvamizi wa tembo unaosababisha uharibifu wa mazao na kuhatarisha usalama wa wananchi.

Dk. Kijaji ametoa maelekezo hayo akiwa katika ziara yake mkoani Kagera, kufuatia ombi la Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, aliyewasilisha changamoto ya uvamizi wa tembo katika kata za Rugu, Rugera, Kihanga, Nyakabanga na Nyakakika.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyakabanga, Waziri Kijaji amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua za kudumu kukabiliana na kero hiyo kwa wananchi wanaoishi jirani na Hifadhi za Taifa za Burigi-Chato, Ibanda-Karagwe na Rumanyika-Kyerwa. Ameongeza kuwa wananchi ambao mazao yao yameharibiwa na tembo watapatiwa fedha za kifuta jasho zenye jumla ya Sh milioni 39 ndani ya siku saba.

Katika ziara hiyo, Waziri Kijaji pia aliweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Nyakakika. Serikali tayari imetoa Sh milioni 250 kwa ajili ya kuanza ujenzi huo na imetenga shilingi milioni 250 nyingine kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27 ili kukamilisha mradi huo.

Awali, Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, alimshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha wakulima wa Wilaya ya Karagwe na Mkoa wa Kagera kuendelea kunufaika na zao la kahawa kupitia kuimarika kwa bei ya zao hilo kila msimu.

Mbunge huyo pia alizungumzia hali ya Barabara ya Nyakahanga–Nyabiyonza–Nyakabanga–Nyakakika hadi Bweranyange yenye urefu wa kilomita 96.

Alisema barabara hiyo bado ni ya changarawe, huku maeneo korofi yakiwa tayari yamewekewa lami. Ameeleza kuwa awali barabara hiyo ilikuwa ikitengewa shilingi milioni 150 kupitia TARURA, lakini sasa imepandishwa hadhi na itasimamiwa na TANROADS, ambayo imetenga bajeti ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya uboreshaji wake.

Waziri Kijaji, ambaye pia ni Mlezi wa Mkoa wa Kagera, anaendelea na ziara yake ya kikazi katika halmashauri zote za mkoa huo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button