Sh bilioni 2 zakabidhiwa kwa wanufaika wa utalii

MOROGORO: MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imekabidhi Sh bilioni 2.47 kwa wanufaika wa mapato yatokanayo na shughuli za utalii kwa mwezi Julai 2026.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TAWA mkoani Morogoro, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Mlage Kabange, amesema Sh billioni 1,74 zimeelekezwa kwa Jumuiya 11 za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs); Sh millioni 354.94 kwa vijiji 18 na Sh millioni 379.2 kwa halmashauri 21 za wilaya.

Kabange amesema fedha hizo ni sehemu ya mapato yatokanayo na utalii ambayo hurejeshwa kwa jamii kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi na kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mbali na hayo amesema katika mwaka wa fedha 2025/26 pekee, jumla ya Sh bilioni 12.17 zilitolewa kwa wanufaika wa shughuli za utalii.

Licha ya fedha hizo, TAWA imekabidhi ndege nyuki 27 kwa ajili ya kusaidia udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu ambapo ndege 20 zimetolewa kupitia Mfuko wa Wanyamapori Tanzania (TWPF) mbili kutoka Bushman Safari Trackers Limited na tano kutoka TAWA.

Katika kuimarisha zaidi udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu, TAWA imeongeza askari wapya 661 na kuwezesha Askari wa Vijiji 187 kushiriki katika shughuli hizo, sambamba na kuimarisha matumizi ya vitendeakazi na teknolojia.

Kabange amesema hatua hizo zinalenga kuhakikisha jamii zinapata manufaa ya moja kwa moja kutokana na uhifadhi, kuongeza ushiriki wa wananchi, kupunguza migongano kati ya binadamu na wanyamapori na kuchochea shughuli za kiuchumi.

Aidha, TAWA imetangaza namba maalum ya “TAWA NA JAMII” – 0800750440, kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano kati ya Mamlaka na wananchi katika kutoa taarifa na kuwasilisha changamoto zinazohusiana na shughuli za TAWA.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

  2. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button