Dk Sajad apongeza uteuzi, uapisho wa Ndejembi

DAR ES SALAAM: MTAALAM katika Sekta ya Mafuta nchini Dk Sajad Habib Rai amempongeza Makamu wa Rais Ndejembi kwa kuapishwa kwake kushika nafasi hiyo huku alimtabiri mambo mengi katika majukumu yake ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan
Akizungumza Jijini Dar es Salaam siku moja baada ya uapisho wa Makamu Rais huyo Ikulu ya Cha Chamwino, Dodoma, Dk Sajad amesema ana aimani kubwa na Kiongozi huyo huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi wa Ndejembi.
Dk Sajad ambaye ni Meneja Mkazi wa Mansoor Industries nchini, amesema Hana shaka na uwezo wa Ndejembi katika Uongozi akisisitiza kuwa kwa sifa na uwezo alionao ni msaada tosha katika usaidizi kwa Dk Samia Suluhu Hassan.
” Kwa kipindi kifupi alichohudumu katika Wizara ya Nishati kwa nafasi ya Uwaziri , Mheshimiwa Ndejembi amekuwa mtu muhimu aliyesimama kikamilifu katika kuahughulikia masuala mbalimbali, hii ni sifa ambayo siyo kila Kiongozi anayo” amesema Dk Sajad
Amesema hatua ya Rais Samia Hassan kumteua na baadae jina lake kupitishwa na Bunge, kunatokana uwezo wake hatua iliyomfanya kiongozi huyo Mkuu wa nchi kujenga imani dhidi yake hivyo anapaswa kuendelea kumuonesha imani hiyo wakati huu anapomsaidia katika majukumu makubwa zaidi Kiongozi.
Mtaalamu huyo wa Nishati pamoja na Mawasiliano aliyeisaidia Serikali katika ‘upigaji mafuta’ bandarini kupitia ubunifu wake wa mfumo maalumu wa udhibiti wa mafuta (BIL) amewataka wananchi kumuamini Ndejembi sambamba na kumpa ushirikiano wakati huu anapotekeleza wajibu wake.
Pamoja na wananchi Dk Sajad pia amewataka watendaji wote wa Serikali, Wabunge pamoja na wafanyabiashara nchini wakiwemo waliomo katika sekta ya mafuta kuendelea kumuunga mkono Makamu wa Rais Ndejembi ili aweze kutimiza kikamilifu majukumu yake ya kumsaidia Rais Samia na taifa kwa ujumla.
Ndejembi ambaye amehudumu katika nafasi mbalimbali za utumishi pamoja na uongozi ikiwemo ya Waziri wa Utumishi baadae Waziri wa Nishati ameapishwa jana kushika nafasi hiyo ya Makamu wa Rais baada ya mtangulizi wake Dk Emmanuel Nchimbi kujiuzuru hivi karibuni.



