Wadau waweka mkakati Kukabiliana na biashara haramu

MOROGORO; Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala, amefungua warsha ya kukabiliana na biashara haramu ya bidhaa za tumbaku iliyofanyika mkoani Morogoro.
Warsha hiyo imehusisha viongozi wa TCC Plc, maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, maofisa viunganishi wa INTERPOL na wadau wengine.
Warsha hiyo ililenga kuimarisha uelewa, ushirikiano na juhudi za pamoja za kukabiliana na biashara haramu inayohatarisha uchumi wa taifa, mapato ya serikali na biashara halali.



