Sheria 21 zapendekezwa kufanyiwa marekebisho

DODOMA; Serikali imewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2026) ambapo sheria 21 zinapendekezwa kufanyiwa marekebisho.
Akiwasilisha muswada huo bungeni leo Septemba 1, 2026, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, amesema marekebisho ya sheria ni miongoni mwa hatua muhimu za Serikali katika kuweka mazingira wezeshi ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Amezitaja sheria hizo kuwa ni Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu, Sura ya 423, Sheria ya Nguvu za Atomu, Sura ya 188 na Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, Sura ya 197.
“Sheria ya Majina ya Biashara, Sura ya 213; Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80; Sheria ya Kampuni, Sura ya 212; Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20, Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95; Sheria ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Sura ya 174,” amesema.
Amezitaja nyingine ni Sheria ya Chuo cha Uhasibu Arusha, Sura ya 240; Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1; Sheria ya Usimamizi wa Mahakama, Sura ya 237, Sheria ya Baraza la Vijana, Sura ya 441, Sheria ya Usajili wa Hataza, Sura ya 217.
“ Sheria ya Magereza, Sura ya 58, Sheria ya Usimamizi wa Maabara Binafsi za Afya, Sura ya 136, Sheria ya Huduma za Maktaba Tanzania, Sura ya 102, Sheria ya Bodi ya Utalii Tanzania, Sura ya 364; Sheria ya Utalii, Sura ya 65; Sheria ya Alama za Biashara na Huduma, Sura ya 326; na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, Sura ya 148,” amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amesema baada ya mashauriano kati ya Serikali na Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria, amependekeza kuondolewa kwa baadhi ya marekebisho sheria nne, hivyo kubaki sheria 17.
Ametaja marekebisho hayo ni yaliyokuwa yakihusu Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, kutokana na masuala hayo kushughulikiwa kupitia Muswada wa Fedha wa mwaka 2026.
Mengine ni marekebisho yaliyopendekezwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mahakama na Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa yamependekezwa kuondolewa ili kutoa nafasi kwa serikali kuyafanyia kazi zaidi. Bunge limepitisha muswada huo.




This made my morning reading list. It saved me some time digging through other sources. If it’s useful to anyone else, I’ve been following this: https://www.instagram.com/boda8.my Anyway, thanks again.