Sheria za Uchumi wa Buluu ziwe na viwango vya kimataifa

DAR ES SALAAM: MKURUGENZI wa Kitengo cha Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Felix Chakila, amesema Kongamano la Tano la Kimataifa la Uchumi wa Buluu limekuwa fursa muhimu kwa Tanzania kupata mawazo na maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuhusu namna bora ya kuimarisha sekta ya uchumi wa buluu na mali asilia.
Chakila amesema kongamano hilo limewawezesha washiriki kujadili umuhimu wa kuwa na sheria na mifumo ya kisheria itakayowezesha utekelezaji wa uchumi wa buluu kwa ufanisi na kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.
Akizungumza leo, Septemba 7, 2026, katika Kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, Chakila amesema moja ya maazimio yaliyopatikana ni kuhakikisha sheria za Tanzania zinaendana na sheria na viwango vya kimataifa.
Amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuzuia migongano ya kisheria inayoweza kujitokeza katika shughuli za uchumi wa buluu zinazohusisha maeneo ya kimataifa.
“Moja ya maazimio tuliyoyapata ni kuhakikisha sheria za nchi zinaendana na sheria za kimataifa ili kuepusha migongano ya kisheria ambayo inaweza kujitokeza katika anga za kimataifa,” amesema Chakila.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Bahari, Paul Peter Olekashe, amesema Serikali ina mpango wa kuhakikisha uchumi wa buluu unatambulika na kupewa umuhimu zaidi nchini kote kupitia uwekaji wa taratibu, sera na sheria zitakazozingatia manufaa ya sekta hiyo kwa taifa na sekta mbalimbali.
Olekashe amesema baadhi ya sheria zinazohusiana na uchumi wa buluu bado hazieleweki ipasavyo miongoni mwa wananchi kutokana na ukosefu wa uelewa kuhusu faida na umuhimu wa sekta hiyo.
Amesema makongamano kama hilo ni muhimu katika kuongeza uelewa kwa wananchi na wadau kuhusu fursa zilizopo katika uchumi wa buluu pamoja na namna zinavyoweza kutumika katika kuchochea maendeleo ya taifa.
Naye Kamishna wa Sheria, Katiba na Utawala Bora kutoka Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini (TAIRISO), Aron Nzelela, amesema wametembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria katika kongamano hilo kwa lengo la kujifunza kuhusu huduma zinazotolewa na wizara hiyo na kupata uelewa zaidi kuhusu utekelezaji wa Katiba na sheria nchini.
Nzelela amesema kupitia ziara hiyo wameweza kutambua kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Katiba na Sheria katika kusimamia Katiba, sheria za nchi pamoja na sheria zinazohusiana na masuala ya bahari.
Amesema wizara hiyo pia imekuwa kinara katika kuendesha mpango wa msaada wa kisheria wa Mama Samia, ambao umekuwa ukitoa msaada kwa wananchi katika maeneo ya mijini na vijijini.
Kwa mujibu wa Nzelela, juhudi hizo zina mchango mkubwa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kisheria na kutambua haki zao.
Amesema falsafa ya Wizara ya Katiba na Sheria ni kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com