Mtangazaji Misri ahukumiwa kifo

MISRI: Mtangazaji wa televisheni nchini Misri, Sarah Khalifa, ni miongoni mwa watu 12 waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa kutokana na kuhusika katika mtandao wa biashara ya dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Al-Ahram, Mahakama ya Jinai ya Cairo Jumamosi iliwahukumu washtakiwa hao 12 kunyongwa na kuwatoza faini ya pauni za Misri 500,000, sawa na takribani dola za Marekani 9,800 kila mmoja.

Washtakiwa hao walituhumiwa kuunda genge la uhalifu lililojihusisha na kuagiza bidhaa zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya kwa ajili ya biashara, pamoja na kumiliki silaha za moto bila leseni.

Mbali na hukumu hiyo, watu wengine tisa walihukumiwa kifungo cha maisha, huku washtakiwa saba wakiwa wameachiwa huru baada ya mahakama kuwakuta hawana hatia.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button