Tanzania, DR Congo wakubaliana kuwarejesha wakimbizi

LUBUMBASHI: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), zimeazimia kuanza mchakato wa kuwarejesha wakimbizi wa DRC wanaohifadhiwa nchini Tanzania ambao wako tayari kwa hiari yao kurejea nchini kwao.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati akihutubia Mkutano wa Kamisheni ya Pande Tatu (Tripartite Commission Meeting) uliofanyika jijini Lubumbashi leo

Ayoub amesema Tanzania itaendelea kuhakikisha wakimbizi wanaoamua kurejea nchini kwao wanafanya hivyo kwa hiari na utaratibu wa kuwarejesha utazingatia usalama na utu wao na pia Tanzania haitawahamasisha au kuwashawishi wakimbizi hao kurejea nyumbani.

Ayoub ameeleza kuwa kwa wale ambao bado hawajawa tayari kurejea DRC, Tanzania itaendelea kuwapa hifadhi na kuwahudumia kulingana na rasilimali zilizopo, katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.

Aidha, amesisitiza kuwa kuanza kwa mchakato wa urejeshaji wa hiari hakutaizuia Tanzania kuendelea kupokea waomba hifadhi wapya wanaokimbilia Tanzania kutokana na ukosefu wa usalama katika baadhi ya maeneo ya DRC.

Aidha, ametoa Wito kwa viongozi wa DRC kutembelea Kambi ya Nyarugusu ili kukutana moja kwa moja na raia wao, kusikiliza mahitaji yao ili wajisikie kuwa sehemu ya taifa lao. Amesema ziara hizo hazipaswi kuwa za kuwashawishi wakimbizi kurejea, bali kujenga uhusiano na matumaini kwa raia hao.

 

Kadhalika, pande zote zimekubaliana kuweka mazingira wezeshi kwa wakimbizi waliotayari kurejea nchini kwao ili kuungana na familia zao na kushiriki katika ujenzi na maendeleo ya taifa lao.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button