Watu 94,000 wakimbia makazi mapigano Yemen

YEMEN: Takribani watu 94,000 wamekimbia makazi yao nchini Yemen tangu mapigano kati ya waasi wa Houthi na vikosi vya Serikali yalipozidi kuwa makali mwezi huu, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni majimbo ya Taiz na Lahj, ambako zaidi ya watu 48,000 wamekuwa wakikimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo.

IOM imetoa wito wa kupatikana kwa msaada wa haraka kwa ajili ya kuwapatia makazi, maji safi na huduma za usafi wa mazingira familia zilizolazimika kuondoka kwenye makazi yao.

Wakati huo huo, zaidi ya watu 2,000 wamevuka bahari na kuingia nchini Djibouti, wakitumia boti ndogo na kufika katika maeneo ya pwani ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Timu za IOM zimekuwa zikisaidia wahamiaji hao kufika ufukweni, huku zikiwapatia chakula na makazi ya dharura. Wanawake na watoto wameonekana wakitafuta hifadhi dhidi ya joto kali chini ya mahema ya muda yaliyowekwa kando ya ufukwe.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button