Madiwani Kibiti wataka kamera kudhibiti mapato

PWANI: BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti limesisitiza ufungaji wa kamera katika baadhi ya vyanzo vya ukusanyaji mapato Kama kituo cha mabasi kibiti na mageti ya ya ukusanyaji ushuru ili kuzuia mianya ya uvujaji wa mapato ndani ya halmashauri ya kibiti.
Agizo hilo limetolewa Septemba 16, 2026 na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhe. Malela Tokha, wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Robo ya Nne.

“Kwa mwaka huu tumekubaliana kukusanya kiasi cha Sh bilioni 4.1. Tushikamane kwenye jambo hili kwa sababu bado makusanyo yetu hayaridhishi. Hivyo basi tushikamane kwa pamoja ili tuweze kukusanya mapato stahiki na kamera zikifungwa itatusaidia kuziba mianya ya upotevu wa mapato,” amesema.
Aidha, baraza hilo limeagiza katika baraza lijalo iwasilishwe sheria ndogo ili ziweze kufanyiwa marekebisho na kutumika.
Pia, limeagiza katika vikao vijavyo madiwani wote kutumia vishikwambi na kuachana na matumizi ya karatasi ili kuendana na teknolojia.

Akiwasilisha salamu za Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo, amewataka madiwani kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuondoa manung’uniko kwa wananchi.
“Miradi mingi inayotekelezwa imo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Mfano mzuri ni lile soko. Ni wazi wananchi wanashindwa kunipiga mawe kwa sababu mimi ni mzee mwenzao, lakini wanatembea na machungu moyoni. Hivyo tuhakikishe linakamilika,” amesema.

Kolombo amesema zaidi ya watoto 5,000 wanatarajiwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2028, hivyo changamoto ya uhaba wa madarasa na matundu ya vyoo inapaswa kutatuliwa kwa wakati endapo fedha zitahidhinishwa kwa wakati.





❤️ Wasichana warembo na wenye hamu ya kimapenzi kutoka kote duniani wanakungoja; jiunge hapa ……………> https://da.gd/girls66