Mbeya wajiweka sawa kukabiliana na El Nino

MBEYA; SERIKALI imetoa vifaa vya ujenzi wa barabara kwa ajili ya maandalizi ya kukabiliana na mvua za El Niño mkoani Mbeya.

Vifaa hivyo,ambavyo ni  makaravati ya chuma vitatumika katika barabara kuu sita zinazounganisha Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo,  Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, amesema vifaa hivyo vimeletwa kwa ajili ya kudhibiti na kurekebisha miundombinu ya barabara, iwapo mvua hizo zitasababisha madhara kwenye miundombinu hiyo.

“Tumejipanga kikamilifu kuhakikisha barabara zinapitika wakati wote na shughuli za usafirishaji wa watu na bidhaa haziathiriki katika kipindi chote cha mvua,”amesema Mhandisi Bishanga.

Agosti 18, mwaka huu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitabiri uwepo wa mvua za El Nino kwa kuwepo ongezeko la mvua za vuli (Oktoba – Desemba) kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi nchini.

Mvua hizo zinatarajia kuanza wiki ya nne ya Septemba hadi wiki ya kwanza ya Oktoba 2026 katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria. Hii itasambaa taratibu katika maeneo mengine katika Oktoba 2026.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button