Mawakala 120 Marekani wavutiwa utalii Tanzania

MARA: Mawakala wa utalii 120 kutoka nchini Marekani wameonyesha kuvutiwa na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini Tanzania, hususan mandhari ya kuvutia, wanyamapori, na urithi wa utamaduni wa kipekee.

Tukio hilo limejidhihirisha katika usiku wa Novemba 7, 2025 kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara, iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kuwakaribisha mawakala hao waliowasili nchini kwa ziara ya kutembelea vivutio vya utalii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Excellent Guide Tours and Safaris, Justin Alfred, amesema; “Tumevutiwa sana na mandhari ya Tanzania, hasa wanyamapori kama tembo, twiga, simba na nyati. Nchi hii ni salama, wananchi wake ni wakarimu, watalii wasisite kuja kuitembelea.”

Amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha Tanzania inatambulika zaidi duniani kama kitovu cha utalii barani Afrika kutokana na urithi wake wa asili, utamaduni na vivutio vya kipekee.

Kwa upande wake, Patricia Walker kutoka kampuni ya Nexion Travel ya Marekani, amesema kutembelea Tanzania ilikuwa ndoto yake tangu akiwa na umri wa miaka mitano, hususan kuona Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Naye, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Stephano Msumi, amewashukuru mawakala hao kwa kuichagua Tanzania kama sehemu ya kujionea vivutio vya asili, na kuwahimiza wawe mabalozi wazuri wa utalii watakaporejea nchini kwao.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting website

    More Details For Us→→  http://www.job40.media

  4. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting website

    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→ http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button