‘AFCON 2027 ni dhahabu kwa wafanyabiashara’

DAR ES SALAAM: Wafanyabiashara nchini wametakiwa kuanza kujiandaa mapema kutumia fursa zitakazotokana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, kwa kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kuongeza shughuli za kiuchumi katika sekta mbalimbali.
Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Masoko wa Photons Energy, Roman Shayo, amesema AFCON siyo tukio la michezo pekee, bali ni fursa kubwa inayoweza kugusa moja kwa moja biashara za sekta mbalimbali, ikiwemo utalii, usafirishaji, hoteli, teknolojia, ujenzi na biashara ndogo ndogo.
Shayo amesema uwekezaji unaofanywa na serikali katika maandalizi ya AFCON unatokana na ukubwa wa fursa zinazoweza kupatikana, hivyo wafanyabiashara wanapaswa kuwa na mtazamo chanya na kuanza kupanga mapema namna watakavyonufaika.

Amesema wamiliki wa hoteli na nyumba za kulala wageni wanaweza kutumia kipindi hiki kuboresha miundombinu na huduma zao, huku wanaojihusisha na usafirishaji wakitakiwa kuongeza uwezo wao ili kukidhi mahitaji yatakayoongezeka wakati wa mashindano hayo.
Kwa wafanyabiashara wadogo, Shayo amesema AFCON inaweza kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma, hivyo ni muhimu kujiandaa kwa kuongeza uzalishaji kulingana na mahitaji ya soko.
“AFCON inapokuja siyo mpira tu. Fursa zake ni nyingi, zinagusa teknolojia, utalii, hoteli, mbuga, mama mboga, barabara, umeme na kila kitu,” amesema Shayo.
Amesema Serikali tayari imefanya sehemu yake kwa kuweka mazingira na kuwekeza katika maandalizi, hivyo jukumu la wafanyabiashara sasa ni kutambua fursa na kujiandaa kuzitumia.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily…………
.
More Details For Us→→→→ https://Www.Payathome9.Com
I conceive this website holds some real great information for everyone. “To be able to be caught up into the world of thought — that is being educated.” by Edith Hamilton.