Akili unde kupima saratani ya matiti

TEKNOLOJIA ya akili bandia (AI) imeanza kutumika katika uchunguzi wa saratani ya matiti nchini, baada ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) kupata mashine ya kisasa ya mammography yenye uwezo wa kusaidia kubaini mabadiliko ya awali ya ugonjwa huo.

Mashine hiyo mpya yenye thamani ya Sh milioni 600, inatumia teknolojia ya kisasa ya X-ray ya matiti na imeunganishwa na mfumo wa akili bandia unaosaidia wataalamu kubaini maeneo yanayoweza kuwa na dalili za saratani na yanayohitaji uchunguzi zaidi. Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk. Diwani Msemo, amesema teknolojia hiyo itaongeza uwezo wa taasisi katika kugundua saratani ya matiti mapema na kuwawezesha wagonjwa kuanza matibabu kwa wakati.

Amesema mashine hiyo ina uwezo wa kutambua maeneo yenye mashaka wakati wa uchunguzi na kumwelekeza mtaalamu sehemu inayohitaji kuangaliwa kwa umakini zaidi.“Ni mashine ya kisasa yenye akili bandia ambayo wakati inafanya screening ina uwezo wa ku-identify baadhi ya maeneo yenye matatizo na kumwonyesha msomaji wa picha hapa kuna shida, hivyo aangalie kwa makini eneo husika,” amesema.

Dk. Msemo amesema mashine hiyo pia ina uwezo wa kusaidia kuchukua sampuli ya tishu, maarufu kama biopsy, pale inapobainika kuwa kuna eneo linalohitaji uchunguzi zaidi. Amefafanua kuwa biopsy ni mchakato wa kuchukua sampuli ya tishu mwilini na kuipeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini iwapo ina seli za saratani. SOMA: Saratani ya Matiti Yazidi Kuwa Tishio

Kwa mujibu wa Dk. Msemo, takribani asilimia 10 hadi 12 ya wagonjwa wanaofika ORCI wanakuwa na saratani ya matiti, ambayo ni saratani ya pili kwa ukubwa baada ya saratani ya mlango wa kizazi. Amesema matumizi ya mashine hiyo yataunganishwa na huduma nyingine za kisasa zinazotolewa ORCI, ikiwamo PET Scan, inayosaidia kubaini iwapo saratani imesambaa katika sehemu nyingine za mwili.

Aidha, Dk. Msemo amesema ORCI imepanga kuwapeleka wataalamu watatu nchini Uturuki kwa ajili ya kupata mafunzo zaidi kuhusu matumizi ya mashine hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuongeza uwezo wa wataalamu nchini. Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Radiolojia na mtaalamu wa uchunguzi wa matiti, Dk. Anganile Kalinga, amesema mashine hiyo inaweza kubaini mabadiliko madogo ambayo wakati mwingine hayaonekani kupitia ultrasound.

Amesema miongoni mwa mabadiliko hayo ni yale madogo ya muundo wa titi ambayo yanaweza kuwa dalili za awali za saratani.“Mashine hii inaweza kuona dalili za mwanzo kabisa ambazo tunaweza kuziita microcalcification na mabadiliko madogo ambayo hata ukifanya ultrasound unaweza usiyaone,” amesema.

Dk. Kalinga amewataka wanawake wenye umri wa miaka 40 na kuendelea kutosubiri hadi waone uvimbe ndipo wafike hospitalini, bali wafanye uchunguzi wa matiti mara kwa mara. Amesema wanaume pia wanaweza kupata saratani ya matiti, ingawa kiwango chake ni kidogo ikilinganishwa na wanawake. Amesisitiza kuwa wanaume wanapaswa kufika hospitalini iwapo watagundua mabadiliko yoyote katika matiti ili kufanyiwa uchunguzi na kupata ushauri wa kitaalamu.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

  2. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills. This is what I do…..  http://www.work27.info

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button