Askari wawili wafariki kwa kugongwa gari kwenye zebra

PWANI; Polisi mkoani Pwani inamshikilia dereva Josia Arute (34) mkazi wa Mlandizi, Kibaha kwa tuhuma za kugonga na kusababisha vifo vya askari wawili wa jeshi hilo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani, Salim Morcase imeeleza kuwa askari hao walifariki dunia baada ya kugongwa na gari kwenye kivuko cha waenda kwa miguu (zebra), walipokuwa wakivusha watu Agosti 25, 2026 saa moja usiku, Maili Moja, Wilaya ya Kibaha, Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Morogoro.

Taarifa imewataja askari hao ni Izdory Michael aliyefariki papo hapo na Rehema Magawa aliyefariki siku iliyofuata alipokuwa akipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Pwani Tumbi.

Dereva huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Noah, namba za usajili T 804 ERM likiwa linatoka Dar es Salaam kuelekea Mlandizi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button