Dk Mwigulu asimikwa kuwa Kanoni Mlei Kanisa Anglikana Tanzania

TANGA; Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, leo Jumapili, Oktoba 4, 2026, amesimikwa rasmi kuwa Kanoni Mlei (Lay Canon) wa Kanisa Anglikana Tanzania katika ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kristu Mfalme, Chanika, Dayosisi ya Handeni, mkoani Tanga.
Dk Mwigulu amesimikwa katika wadhifa huo katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu kwa Kasisi Canon Charles Mika Lundu kuwa Askofu wa Dayosisi ya Handeni. Dk Mwigulu alishiriki ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
Waziri Mkuu alitunukiwa cheo cha Kanoni Mlei na Kanisa Anglikana Tanzania, chini ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk Maimbo Mndolwa, Juni 21, 2026, katika Harambee ya kukamilisha mradi wa jengo la Kitega Uchumi cha Kanisa Anglikana Tanzania iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, Jimbo la Dodoma.
Kanisa Anglikana Tanzania lilimtunuku Waziri Mkuu cheo hicho kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha na kufanikisha uchangishaji wa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na vitega uchumi vya Kanisa hilo, tangu alipokuwa akitumikia nyadhifa mbalimbali za serikali na kijamii.
Kutunukiwa cheo hicho na hatimaye kusimikwa rasmi leo katika ibada iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dk Maimbo Mndolwa, kumemfanya Waziri Mkuu kuungana na viongozi wengine wa Serikali waliowahi kutunukiwa wadhifa huo, huku akiwa Kanoni Mlei wa kwanza kutoka nje ya dhehebu la Anglikana, kwa mujibu wa taarifa hiyo.
 
Viongozi wengine waliowahi kutunukiwa cheo cha Kanoni Mlei (Lay Canon) ni pamoja na Spika mstaafu, Hayati Job Ndugai; Jaji Mkuu Mstaafu, Hayati Augustino Ramadhani; na Profesa Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu).
 
Wengine ni Baraka Leonard, Katibu wa Bunge, pamoja na Gerald Mweli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo.
 
Kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Anglikana, Kanoni Mlei ni cheo cha heshima katika Kanisa hilo, ambacho miongoni mwa majukumu yake ni kutoa ushauri na kuwa mlezi wa uongozi wa juu wa Kanisa

Habari Zifananazo

5 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

  2. I do not think that having many references is enough to demonstrate good research. The sources need to be relevant to the question and used in a way that shows their relationship https://domycourseworkforme.com/ to the subject. Writemyliteraturereview.com was useful to me as a reference point when considering how to present these relationships in a literature review. It also helped me think more carefully about the order of the sections.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button