MAKAMU Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania PHAM (T), Askofu Julias Bundala amehimiza ushirikiano wa wananchi na vyombo vya ulinzi kukomesha uhalifu wa makundi ya vijana maarufu kwa jina la panya road.
Askofu Bundala alisema hayo jana wakati wa mahojiano na waandishi wa habari Dodoma kuhusu vikundi hivyo vya kihalifu ambavyo vimekuwa tishio kwa raia na mali.
Alisema vikundi hivyo vinaishi kwenye jamii hivyo kukiwapo ushirikiana kati ya viongozi wa serikali za mitaa, kata na wilaya, upo uwezekano mkubwa wa kuvikomesha.
“Makundi hayo ambayo wengi wao ni vijana wenye umri mdogo,wanatoka kwenye familia za wazazi na walezi kwa maana hiyo wakitoa ushirikiana, panya road watadhibitiwa na kukomeshwa,” alisema.
Alishauri viongozi wa ngazi za mitaa kuanzisha makundi ya ulinzi shirikishi kuimarisha ulinzi kwenye maeneo mbalimbali.