CCM Tanga kuweka nguvu utatuzi migogoro ya ardhi

 CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga,  kimejipanga kuhakikisha kinamaliza migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali mkoani humo, ambayo imekuwa ikileta athari kwa wananchi.

 Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa Rajab Abdulrahman, wakati akizungumz na waandishi wa habari kueleza mikakati ya uongozi wake ndani ya miaka mitano.

 Amesema mkoani humo kumekuwa na migogoro mingi ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu, ambayo imeleta madhara kwa wananchi ikiwemo vifo.

 “Kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, tutakaa kwa pamoja kuona namna nzuri ya  kutafuta suluhisho la kuondoa migogoro hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa ipo katika wilaya za Handeni na Kilindi,” amesema Mwenyekiti huyo.

 Amesema miongoni mwa malengo aliyokuwa nayo ni kuhakikisha chama hicho kinakuwa kimbilio kwa wananchi wanyonge, kwa kuwa sehemu ya watetezi wao na kuwa sehemu ya suluhisho kutokana na changamoto zinazowakabili. 

“Katika uongozi wangu kwa miaka mitano nikishirikiana na viongozi wote tunataka CCM iendelee kuwa kimbilio la wananchi wote wanaoishi mkoa wetu wa Tanga, kila mmoja atapata haki yake hakuna atakayeonewa, tutaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ipasavyo tena kwa vitendo, ” amesema Rajab.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button